ITALIA

Klabu ya Napoli yamtolea macho kocha wa muda wa klabu ya Chelsea Rafael Benitez

Rais wa timu ya soka ya Napoli Aurelio De Laurentiis amekutana na kocha wa muda wa klabu ya Chelsea Rafael Benitez katika jitihada za kumshawishi kuiongoza klabu ya Serie A taarifa kutoka nchini Italia zimearifu. 

Rais wa klabu ya Napoli Aurelio De Laurentiis
Rais wa klabu ya Napoli Aurelio De Laurentiis noi.napoli.it
Matangazo ya kibiashara

Klabu ya Napoli ilitangazwa kushika nafasi nyuma ya klabu ya Juventus baada ya msimu kumalizika jana Jumapili , hatua inayomaanisha kuwa klabu hiyo imefuzu kushiriki ligi ya mabingwa msimu ujao.

Haja ya klabu ya Napoli kupata kocha mpya ni kubwa kufuatia aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Walter Mazzarri kuthibitisha kuondoka kwake katika klabu hiyo jana Jumapili.

Benitez ambaye amewahi kuwa meneja wa Liverpool pia amewahi kuwa kocha nchini Italia, akichukua nafasi ya Jose Mourinho baada ya kocha huyo Mreno kuiongoza Inter Milan katika ligi ndogo na Ligi ya Mabingwa.