Nadal na Serena wang'ara mashindano ya Italia Open
Imechapishwa:
Wacheza Tennis Rafael Nadal na Serena Williams wamewaonya wapinzani wao Roger Federer na Victoria Azarenka kujipanga vizuri kuelekea katika mashindano ya French Open kwa kuwa wao ndio watakaoibuka washindi .
Nadal ameonesha mashambulizi yenye kuzaa matunda kwenye mchezo wa tenisi tangu arejee kwenye mchezo huo baada ya kukosekana baada ya ushindi wake wa mara ya saba ndani ya miaka tisa huko Roma na kumwacha mpinzani wake Roger Federer akiwa hana mashaka dhidi yake kuhusu kutwaa taji la French Open kwa mara ya nane.
Wakati ikiwa ni mara ya kwanza kwa Federer kushiriki fainali hizo kwa upande wa Nadal hii ni mara yake ya nane baada ya kumwangusha mbali mpinzani wake Tomas Berdych sikumoja baada ya kumshinda bingwa namba moja duniani Novak Djokovic katika hatua ya robo fainali.
Wakati Federer na Djokovic wakisimama upande wa Nadal, Serena Williams anajiandaa kukabiliana na changamoto yake ngumu kwa kumvaa Victoria Azarenka na bingwa mtetezi wa taji hilo Maria Sharapova.
Baada ya Sharapova kujiondoa kutokana na homa kabla ya robo fainali dhidi yake na Sara Errani wa Italia,Serena alifuzu kutinga katika fainali ambapo Azarenka baada ya kumshinda Errani katika nusu fainali alipata ushindi wa aina hiyo katika fainali.