michezo

Sabine aendeleza ushindi mashindano ya Wimbledon

Mcheza tennis wa Ujerumani Sabine Lisicki
Mcheza tennis wa Ujerumani Sabine Lisicki wallpaperweb.org

Mjerumani Sabine Lisicki amendeleza ushindi wake katika mashindano ya Tennis ya Wimbledon baada ya kumwondosha bingwa namba moja katika mchezo huo duniani Serena Williams hapo jana Jumatatu leo amefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali kwa kumfunga m Estonia Kaia Kanepi kwa seti mbili za 6-3, 6-3 kwenye mchezo wa leo Jumanne . 

Matangazo ya kibiashara

Mchezaji huyo bingwa namba 23 wa Ujerumani pia alifanikiwa kufuzu katika hatua ya nusu fainali mwaka 2011 atakabiliana na bingwa namba nne wa Poland Agnieszka Radwanska, ambaye alikuwa nyuma ya bingwa mtetezi kwa mara ya tano Serena Williams mwaka uliopita, ama atavaana na Li Na wa China kuwania kushiriki Fainali.