Uhispania

Waziri mkuu Uhispania ayakabili maswali ya wabunge kufuatia kashfa ua ufisadi

Waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy.
Waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy. REUTERS/Sergio Perez

 Waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy amekanusha madai ya ufisadi yanayomkabili alipojitokeza mbele ya wabunge kukabili maswali na majibu kufuatia kashfa ya matumizi mabaya ya fedha,kashfa inayotishia chama chake mashuhuri kilichopo madarakani PP.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Rajoy amekabiliwa na maswali kuhusu malipo haramu yaliyofanywa na mhazina wa zamani wa chama chake Luis Barcenas ambapo awali waziri huyo na wanachama wengine walikanusha madai ya kupokea malipo haramu.

Hasira kali ilienea kufuatia madai hayo kugusa maeneo nyeti nchini Uhispania na kusababisha maandamano ya kupinga serikali na wito kwa waziri huyo kujiuzulu.

Waziri Rajoy anajitokeza mbele ya bunge kufuatia vitisho vya kura ya kutokuwa na imani nae,katika maelezo yake ya awali alibainisha kuwa anajitokeza wakati huu kwa vile madai hayo hayana ukweli.

Hivi karibuni kulizuka mapigano kati ya polisi na waandamanaji waliokuwa wakipinga serikali mnamo katikati ya mwezi julai ambapo zaidi ya watu elfu moja walikusanyika nje ya ofisi za makao makuu ya chama cha PP na kukitaka kujiondoa madarakani.