CHINA-NEW ZEALAND

China yaagiza kupitiwa upya kwa bidhaa za maziwa kufuatia hofu ya sumu

Maziwa yanayodaiwa kuwa na sumu
Maziwa yanayodaiwa kuwa na sumu telegraph.co.uk

China imeiagiza kampuni ya madawa ya nchini Marekani Abbott kufanyia mapitio baadhi ya bidhaa nchini humo kufuatia hofu ya sumu iliyotajwa kwenye kampuni kubwa ya maziwa ya nchini New Zealand, Mamlaka nchini humo zimeeleza leo Jumanne. 

Matangazo ya kibiashara

Msimamizi mkuu wa Mamlaka ya uangalizi na ukaguzi wa ubora AQSIQ amesema katika taarifa kuwa shehena mbili za maziwa ya watoto yaliyotengenezwa na Abbot yanahofiwa kuchafuliwa na bakteria aina ya Clostiridium.

Bakteria wa Klostiridium ni bakteria ambao wanaweza kusababisha sumu na maambukizi ambayo yanaweza kusababisha ulemavu na kifo.

Mamlaka hiyo ya uangalizi na ukaguzi wa ubora imeiagiza Abbott kupitia upya bidhaa husika ili kulinda afya ya walaji wa China, imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa mchanganyiko huo wa maziwa maalumu kwa watoto wenye umri kati ya mwaka mmoja na mitatu, uliandaliwa na Fonterra Mei 2 kwa ajili ya kampuni tanzu ya Abbott ya mjini Shanghai.

Fonterra iliweka wazi mwishoni mwa juma kuwa bidhaa hiyo itumikayo kutengeneza maziwa ya watoto na vinywaji laini ilikuwa imechafuliwa na bakteria.