Uhispania

Mtuhumiwa wa ubakaji nchini Morocco atiwa nguvuni Uhispania

Mtuhumiwa wa ubakaji Daniel Galvana Vina
Mtuhumiwa wa ubakaji Daniel Galvana Vina teinteresa.es

Raia wa Uhispania aliye hukumiwa kifungo cha miaka 30 jela nchini Morocco kwa kosa la kumbaka mtoto na kuachiwa huru Jumapili iliyopita amekamatwa na kutiwa nguvuni nchini Uhispania. 

Matangazo ya kibiashara

Maafisa nchini Uhispania wamethibitisha Daniel Galvan Vina, ambaye aliachiwa huru kwa msamaha wa kifalme alitiwa kizuizini huko Murcia.

Maafisa nchini Morocco wamedai makosa yalifanyika kufuatia hatua ya kumsamehe Daniel Vina ambapo mfalme Mohamed hakutambua chanzo halisi cha makosa ya Daniel Galvan Vina.

Mfalme Mohamed amempiga kalamu mkuu wa magereza na kubatilisha msamaha wake.

Galvan,alikutwa na hatia ya kuwabaka jumla ya watoto 11 wenye umri kati ya miaka minne na kumi na tano ambapo mnamo mwezi Septemba mwaka 2011 alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 akiwa gerezani.