UTURUKI-PKK

Waziri mkuu wa Uturuki alituhumu kundi la PKK kutoheshimisha makubaliano

Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan
Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan REUTERS/Dado Ruvic

Waziri mkuu wa Uturuki recep Tayep Erdowan amewatuhumu waasi wa ki kurdi wa kundi la PKK kwa kutoondoka nchini Uturuki kama ilivyokuwa inatrajiwa, na kutupilia mbali uwezekanoi wowote wa kutowa msamaha wa jumla.

Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo amesema ahadi zilizotolewa na kundi hilo la kuondoka katika ardhi ya Uturuki haikutekelezwa ispokuwa pekee asilimia 20 ya waasi wa kundi hilo ndio walioondoka ambapo wengi ni wanawake na watoto.

Katika mazungumzo yaliofanyika mwaka 2012 na kiongozi wa kundi la PKK Abdallah Ocalan aliekatika kifungo cha maisha, waasi wa PKK walitangaza kusitisha vita mwezi March mwaka 2013 na kuanza kuondoka mwezi Mei, huku wakiita serikali kutowa msahama wa jumla utaomuhusu pia kiongozi wa kundi hilo.

Waziri Erdowan amesema katika kama hiyo itakuwa ngumu kutekeleza matakwa ya waasi hao wanaotaka kutowa mafunzo ya ki kurdi kwenye shule mbalimbali na kutowa msahama kwa waasi.

Kundi hilo la PKK limetishia kuanza vita tena Septamba Mosi dhidi ya serikali ya Ankara iwapo makubaliano yaliofikwa hayatotekelezwa.

Serikali ya waislam wa kihafidhina inajadili kuhusu muswada wa sheria uhusua makubaliano na kundi la PKK, ambao utapelekwa bungeni na ambao huenda ukapasishwa mwezi Septemba.

Waziri Erdowan ameendelea kusisitiza hakuna swala la msamaha wa jumla na kuongeza kuwa ombi la kundi la PKK la kutaka kutowa mafunzo kwenye shule za serikali na hata shule binafasi halipo kwenye agenda.

Hata hivyo waziri huyo amesema miongoni mwa mabadiliko yatofanywa na serikali yatakuwa ya mshtuko. Hakutaja mabadiliko hayo.

Mzozo wa ki Kurdi nchini Uturuki umegharimu maisha ya watu elfu arobaini tangu mwaka 1984 wakati kundi hilo lilipoanzisha mapambano dhidhi ya serikali.