UKRAINE-Maandamano

Mzozo wa Ukraine waendelea kutokota, kituo cha polisi chadhibitiwa na waandamanaji

Ghasia za jumamosi huko Donetsk nchini Ukraine
Ghasia za jumamosi huko Donetsk nchini Ukraine REUTERS/Gleb Garanich

Waandamanaji wanaounga mkono Urusi wamedhibiti makao makuu ya polisi huko mji wa mashariki mwa Ukraine Kramatorsk vyombo vya habari nchini humo na mashahidi wamebainisha.

Matangazo ya kibiashara

Udhibiti huu uligubikwa na majibizano ya risasi huku polisi wakijilinda wakati washambuliaji wakishambulia jengo hilo.

Majengo mengine kadhaa ya ofisi za serikali yameripotiwa kudhibitiwa huko Donetsk hapo jumamosi.

Makabiliano hayo yanakuja kufuatia kuzuka kwa mvutano kati ya serikali mpya na waandamanaji wanaounga mkono Urusi.

Shinikizo limeongezeka katika majimbo mengine ya mashariki mwa Ukraine baada ya jimbo la Crimea kupiga kura ya kujiondoa Ukraine na kujiunga na Urusi.