UKAINE-URUSI-G7-Vikwazo

Marekani yawachukulia vikwazo viongozi 7 wa Urusi

Waasi wa Ukraine wanaounga mkono serikali ya Urusi wakiwa mbele ya jengo la manispa ya jiji la Kostiantynivka, ambayo wanaishikilia tangu jumatatu hii asubuhi, aprili 28 mwaka 2014.
Waasi wa Ukraine wanaounga mkono serikali ya Urusi wakiwa mbele ya jengo la manispa ya jiji la Kostiantynivka, ambayo wanaishikilia tangu jumatatu hii asubuhi, aprili 28 mwaka 2014. REUTERS/Marko Djurica

Marekani imewawekea vikwazo viongozi saba wa Urusi pamoja na mashirika 17 ya Urusi yaliyo karibu na rais wa Urusi Vladimir Putine kwa kile Marekani inasema ni kutokana na vitendo vya uchokozi dhidi Ukraine.

Matangazo ya kibiashara

Washington inasema itapitia upya masharti ya usafirishaji wa bidhaa zinazohusiana na matumizi ya kijeshi nchini Urusi. Tangazo hilo limetolewa katika mji mkuu wa Ufilipino, Manila, ambako rais wa Marekani anafanya ya kikazi.

Rais wa Marekani Barack Obama akitangaza vikwazo dhidi ya viongozi 7 wa Urusi na mashirika 17 ya Urusi.
Rais wa Marekani Barack Obama akitangaza vikwazo dhidi ya viongozi 7 wa Urusi na mashirika 17 ya Urusi. REUTERS/Kim Hong-Ji

Wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels nchini Ubelgiji, kujadili hali ya kisiasa na usalama nchini Ukraine na kutangaza majina mapya ya viongozi wa juu wa Urusi watakaowekewa vikwazo.

Marekani na Mataifa tajiri ya G7 yanapanga kuiwekea Urusi vikwazo kwa tuhuma kuwa inendelea kusababisha kudorira kwa usalama nchini Ukrane.

Wakati huo huo serikali ya Ujerumani imeomba Urusi kulani wazi kukamatwa kwa aangalizi wa Kimataifa wanaozuiliwa na waasi wa Ukraine tangu ijumaa mashariki mwa taifa hilo.

Waasi hao wanasema waangalizi hao ni majasusi wa Majeshi ya nchi za mgaharibi Nato tuhma ambazo waaangalizi hao wamekanusha.

Urusi imeombwa pia kuwashawisi waasi hao ili waweze kuwaachia huru waangalizi hao wakimataifa.

Waasi wa Ukraine wanaounga mkono serikali ya Urusi wakiendelea kuteka majengo ya Serikali, mashariki mwa Ukraine.
Waasi wa Ukraine wanaounga mkono serikali ya Urusi wakiendelea kuteka majengo ya Serikali, mashariki mwa Ukraine. REUTERS/Marko Djurica

Hayo yakijiri waasi 300 wa Ukraine wanaounga serikali ya Urusi, wakiwa na marungu na silaha, huku wakiwa wameficha nyuso zao wamevamiya mapema leo asubuhi Privat benki ya bilionea Igor Kolomoïski, katika mji wa Donetsk (mashariki), ameshuhudia mwanahabari wa shirika la Habari la Ufaransa AFP.

Waasi hao wamekua na mabango waliyoandika “ Kolomoïski adui wa raia!”. Bilionea huyo aliteuliwa hivi karibuni kuwa mkuu wa mkoa jirani wa Dnipropetrovsk.

Kolomoïski, alitangaza hivi karibuni baada ya kuteuliwa kwake, kutoa kitita cha dola 10.000 kwa yeyote yule atakayemkamata muasi anaeunga mkono serikali ya Urusi na kuwakabidhi naye viongozi ili ahukumiwe, lakini, hadi sasa jauli hio haijafanyiwa kazi.

Kolomoïski aliwahi kumshambulia kwa maeno makali rais wa Urusi Vladimir Putine, na kumchukulia kama “tapeli”.

Urusi ilinunua mwanzoni mwa mwezi wa Aprili kampuni ya Urusi inayomilikiwa na Privat Benki, ambayo ni benki ya kwanza nchini Ukraine.

Mji wa Donetsk unakumbwa na machafuko baada ya waasi hao kuanzisha vurugu wakitaka kujitenga na ukraine, ambapo viongozi wa Ukraine wamekua wakinyooshea kidole cha lawama serikali ya Urusi kuhusika na vurugu hizo.