URUSI-UKRAINE-EU-Diplomasia

Urusi yajiandaa kukabiliana na vikwazo iliyowekewa

Marekani na Umoja wa Ulaya imewawekea vikwazo viongozi wa Urusi na mashirika yaliyokaribu na rais wa Urusi Vladimir Putine.
Marekani na Umoja wa Ulaya imewawekea vikwazo viongozi wa Urusi na mashirika yaliyokaribu na rais wa Urusi Vladimir Putine. REUTERS/Alexei Nikolskiy/RIA Novosti/Kremlin/Files

Mzozo wa Ukraine unaendelea kutokota, wakati ambapo Urusi imetishia kujibu dhidi ya vikwazo iliyowekewa na mataifa ya magharibi, huku hali ya taharuki ikiendelea kutanda katika maeneo ya mashariki mwa Ukraine yanayoshikiliwa na waasi wa wanaounga mkono Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo, jitihada za kuwakomboa waangalizi wa kimataifa wanaoshikiliwa mateka katika mji wa Slaviansk hazijafaulu.

Hayo yakijiri waasi wanao unga mkono Urusi wanaendelea na harakati zao za kushambulia na kuteka majengo ya serikali mashariki mwa Ukriane, hususan katika mji wa Kostiantynivka karibu na mji wa Donetsk, baada ya mkuu wa manispa ya jiji la Kharkiv, ambaye anaunga mkono Urusi kujeruhiwa.

Hali ya machafuko inaendelaea nchini Ukraine, baada ya waangalizi wa kimataifa kutekwa nyara mashariki mwa Ukraine.
Hali ya machafuko inaendelaea nchini Ukraine, baada ya waangalizi wa kimataifa kutekwa nyara mashariki mwa Ukraine. REUTERS/Gleb Garanich

Kwa upande wake rais wa Urusi Vladimir Putine anashiriki mkutano katika mji mkuu wa Belarus, MINSK.

Mkutano huo unawajumuisha marais wa Urusi Vladimir Putine, wa Belarus Alexandre Loukachenko na rais wa kazakhstan Noursoultan Nazarbaïev ili kujadili mswada unaotoa na fasi ya kukuza uchumi na kuboresha masuala ya forodha katika mataifa yaliyokuwa yakiunda taifa la zamani la jamhuri ya Urusi kwa kujaribu kujitenga na Umoja wa Ulaya.

Wakati huo huo waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza, Theresa May, anakutana kwa mazungumzo na waziri wa sheria wa Marekani, Eric Holder, pamoja na mwenzao wa Ukraine, Arsen Avakov ili jadili kwa pamoja namna ya kurejesha mali ziliyoporwa katika utawala wa rais wa zamani wa Ukraine aliye ng'atuliwa madarakani Viktor Ianoukovitch, mkutano ambao utadumu siku mbili.