UTURUKI-Maadamano

Uturuki: taharuki yatanda siku ya wafanyakazi

Mabomu ya kutoa machozi yakirushwa kwenye eneo la Taksim, mjini Istanbul, mei mosi mwaka 2014.
Mabomu ya kutoa machozi yakirushwa kwenye eneo la Taksim, mjini Istanbul, mei mosi mwaka 2014. REUTERS/Umit Bektas

Siku ya leo ya wafanyakazi imekumbwa na hali ya taharuki katika mji mkuu wa Uturuki, Istanbul, baada ya mwaka moja nchi hio kukumbwa na hali ya vurugu na maandamano. Maelfu ya raia wmejielekeza mapema leo asubuhi kwenye eneo la Taksim ili kujaribu kuanzisha maandamano dhidi ya serikali ya Recep Tayyip Erdogan.

Matangazo ya kibiashara

Makabiliano makali yametokea mapema leo asubuhi, wakati ambapo polisi iliwatawanya waandamanaji ambao wamekua wakijaribu kukaidi hatua ya serikali ya kukakataza mikusanyiko ya watu kwa sikuya wafanyakazi kwenye eneo la Taksim katika mji wa Istanbul.

Kikosi cha kupambana na ghasia wakitumia magari maalumu yenye mikonga ya kurusha maji wameendesha operesheni ya kuwatawanya waandamanaji ambao wamekua wakijaribu kuondoa kwa nguvu vizuizi viliyokua vimewekwa katika mtaa wa Besiktas ili waweze kujielekeza hadi kwenye eneo la Taksim.

Takriban askari polisi 40.000 walimetumwa eneo la Taksim. Polisi imetumia mabomu ya kutoa machozi, huku zaidi ya waandamanaji 130 wamekamatwa na wengine zaidi ya hamsini wamejeruhiwa vikali.

Makabiliano yamezuka karibu na eneo la Taksim,mei mosi mwaka 2014.
Makabiliano yamezuka karibu na eneo la Taksim,mei mosi mwaka 2014. REUTERS/Murad Sezer

Taksim, ni eneo la ukumbusho wanako kusanyika waandamanaji dhidi ya utawala wa Erdogan, ambalo serikali ilipiga marufuku kwa watu kukusanyika. Eneo hilo limekua limezingirwa tangu mapema asubuhi, huku vizuizi vingi vikiwekwa pembezuni mwake.

Hata hivo waziri mkuu wa Uturuki alitoa tangazo jana jumatano na kuonya kwa yeyote atakaye kamatwa kwenye eneo hlo kwamba atachukuliwa hatua za kisheria.

Lakini Vyama vya wafanyakazi na vyama vya siasa vya mrengo wa kushoto viliwatolea wito wafuasi wao kuendelea na msimamo wao wa kuandamana.

Viongozi wa Ukraine walichukua uamzi wa kupiga marufuku maandamano kwenye eneo hilo la Taksim, baada ya kutokea maandamano makubwa mwezi juni mwaka jana. Viongozi hao wamebaini kwamba maandamano hayo ya mwaka jana yalisababisha vurugu.