UKRAINE-Uchaguzi

Serikali ya Ukraine yajaribu kuboresha mazingira ya kiusalama

Mazungumzo ya kitaifa yaliyo washirikisha wadau wote katika usalama wa Ukraine, mazungumzo ambayo yameandaliwa na serikali.
Mazungumzo ya kitaifa yaliyo washirikisha wadau wote katika usalama wa Ukraine, mazungumzo ambayo yameandaliwa na serikali. REUTERS/Andrew Kravchenko/Pool

Siku kumi kabla ya uchaguzi muhimu wa rais kwa ajili ya hatma ya Ukraine ambayo inakabiliwa na vurugu baada ya waasi wanaunga mkono Urusi mashariki kuamua kujitenga na Ukraine , serikali ya Kiev, imekua ikijaribu kutatua mgogoro wa kisiasa ambao umedhoofisha umoja wa kitaifa.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi wa urais nchini Ukraine umepangwa kufanyika Mei 25, lakini waasi wa miji ya Lougansk na Donetsk mashariki mwa Ukraine wameapa kutoshiriki uchaguzi huo.

Serikali ya Kiev inaungwa mkono na mataifa ya magharibi, huko waasi waliyotangaza kujitenga na Ukraine wakiungwa mkono na Urusi.

Mapigano kati ya jeshi na waasi yanaendelea kurindima mashariki mwa Ukraine karibu mwezi moja sasa, baada ya jeshi kuanzisha operesheni dhidi ya “ugaidi”, lengo hasa ikiwa ni kurejesha mikononi mwa serikali maeneo yanayoshikiliwa na waasi mashariki mwa taifa hilo.

Mapigano kati ya jeshi la Ukraine na waasi wa maeneo ya mashariki amao wanataka miji yao kujitenga na Ukraine.
Mapigano kati ya jeshi la Ukraine na waasi wa maeneo ya mashariki amao wanataka miji yao kujitenga na Ukraine. REUTERS/Gleb Garanich

Hayo yakijiri katibu mkuu wa jumuiya ya kujihami ya mataifa ya magharibi Nato, Anders Fogh Rasmussen anakutana kwa mazungumzo katika mji wa Bratislava na viongozi wa Ukraine, Slovakia , Hungary, Jamhuri ya Czech na Poland. Wakati huo huo , mkuu wa ujumbe wa uangalizi wa jumuiya ya Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (OSCE) nchini Ukraine, Ertuğrul Apakan, anatarajiwa kuhutubia leo mbele ya baraza ya jumuiya hio.

Siku moja kabla, serikali ya kiev imekabiliwa na kibarua kigumu kwa kuandaa mazungumzo ya kitaifa yaliyo washirikisha wadau wote katika usalama wa Ukraine. Marais wawili wa zamani wa Ukraine, wagombea urais, wabunge na ujumbe wa baadhi ya waasi wameshiriki mazungumzo hayo.

Raia wa mji Lougansk, moja ya miji iliyojitenga nchini Ukraine.
Raia wa mji Lougansk, moja ya miji iliyojitenga nchini Ukraine. REUTERS/Vasily Fedosenko

Lakini waasi wa miji ya Donetsk na Lougansk ambao waliopiga kura ya maoni jumapili iliyopita, hawakushiriki mazungumzo licha ya wito uliyotolewa na Urusi.