EU-Uchaguzi

EU: Uchaguzi wawatiya wasiwasi viongozi wa Ulaya

Mkutano wa viongozi wa mataifa ya Ulaya unatazamiwa kufanyika kesho katika mji mkuu wa Ubelgiji Brussels, siku mbili baada ya uchaguzi wa wabunge na viongozi wa baadhi ya taasisi za Umoja wa Ulaya kukamilika.

Francois Hollande akiwa ndani ya gari lake baada ya kupiga kura katika mji waTulle, Mei 25 mwaka 2014.
Francois Hollande akiwa ndani ya gari lake baada ya kupiga kura katika mji waTulle, Mei 25 mwaka 2014. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Vyama vinayounga mkono sera za Umoja wa ulaya vimejinyakulia viti vya ubunge 521 kwa jumla ya viti 751. Hata hivyo baadhi ya vyama kutoka mataifa mbalimbali ya bara la Ulaya vimeonekana kupoteza idadi ya viti na vingine kunufaika ikilinganishwa na bunge linaloondoka. Vyama vidogovidogo ambavyo vilikua haviwakilishwi katika bunge la Ulaya, hatimaye vimejinyakulia viti na sasa vitashiriki katika bunge jipya.

Nigel Farage akifurahia ushindi wa chama chake cha Ukip, katika uchaguzi wa Ulaya.
Nigel Farage akifurahia ushindi wa chama chake cha Ukip, katika uchaguzi wa Ulaya. REUTERS/Luke MacGregor

Uchaguzi huu ni pigo kubwa kwa viongozi wa mataifa ya bara la Ulaya, baada ya vyama vigogo katika baadhi ya mataifa kupoteza idadi ya viti vya ubunge, huku vyama ambavyo vilikua kwa kipindi kirefu havishiriki katika bunge la Ulaya vikijinyakulia viti katika taasisi hio kubwa na muhimu barani Ulaya.

Kwa upande wake waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls, amesema kuridhishwa na matukeo ya uchaguzi huo, huku akibaini kwamba kuna uwezekano bara la Ulaya kupiga hatua katika sekta mbalimbali hususan uungwaji mkono wa ukuaji wa uchumi na ajira, ambavyo havikuonekana miaka hiyo ya nyuma.

Chama cha kisoshalisti nchini Hispania, hata chama tawala nchini humo vimepata pigo kubwa katika uchaguzi huo, ambapo chama tawala kimepata viti 14 vya wabunge wakati katika bunge linaloondoka kilikua na wabunge 23 kwa jumla ya bwabunge 54 kutoka taifa hilo la Hispania.

Waziri mkuu wa Italia, Matteo Renzi, ameshiriki katika zoezi la kupiga kura katika mji wa Pontassieve, karibu na mji wa Florence.
Waziri mkuu wa Italia, Matteo Renzi, ameshiriki katika zoezi la kupiga kura katika mji wa Pontassieve, karibu na mji wa Florence. REUTERS/Alessandro Garofalo

La chancelière allemande Angela Merkel a loué la France lundi pour avoir emprunté le chemin des réformes, et a appelé à des politiques de "compétitivité" en Europe pour contrer la montée des partis populistes.

Mapema jumatatu wiki hii, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, amepongeza Ufaransa kwa kuweka mbele njia ya mabadiliko, huku akitolea wito kuweko na siasa za ushindani katika bara la Ulaya ili kukabiliana na kuja juu kwa vyama vya vidogovidogo.