Ukraine

Ukraine: Petro Poroshenko apania kukomesha mapigano

Petro Porochenko rais mtarajiwa wa Ukraine, à Kiev, Mei 25 mwaka 2014.
Petro Porochenko rais mtarajiwa wa Ukraine, à Kiev, Mei 25 mwaka 2014. REUTERS/Gleb Garanich

Mfanyibiashara Petro Porochenko, ambaye alishinda tangu duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Ukraine, anatazamiwa jumatatu hii kutangaza mikakati mipya ya kumaliza vita mashariki na kuongoza taifa hilo kwenye njia itakayopelekea Ukraine kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yakijiri waasi wa mashariki mwa Ukraine wameendelea na harakati zake za kushikilia baadhi ya maeneo ya serikali. Waasi hao wameliteka eneo muhimu, ambako unapatikana uwanja wa ndege wa Donetsk, ambao kwa sasa umefungwa, huku safari za ndege zikiwa zimefutwa.

Siku moja kabla, miji ya Donetsk na Lougansk ili kua na hali ya utulivu, baada ya mapigano makali, ambayo yalisababisha wanajeshi 26 kuuawa. Kungineko nchini Ukraine, raia walishiriki katika zoezi la kupiga kura.

Waasi mashariki mwa Ukraine.
Waasi mashariki mwa Ukraine. REUTERS/Maxim Zmeyev

Katika ngome ya waasi ya Donetsk, hakuna kituo cha kupigia kura kiliofunguliwa. Hapo jana alaasiri takriban watu 2000 walionesha nia yao ya kuunga mkono wanaharakati wa mashariki, ambao wanaungwa mkono na watu wenye silaha ambao wamekua wakificha nyuso zao ili wasiwezi kutambuliwa.

Matokeo rasmi ya ushindi wa Poroshenko, yanatarajiwa kutanagzwa leo Jumatatu baada ya uchaguzi wa urais kufanyika siku ya Jumapili kumchagua kiongozi mpya.

Kura za maoni zinaonesha kuwa Poroshenko ameshinda uchaguzi
huo kwa kupata asilimia 54 ya nusu ya kura ambazo zimesha hesabiwa.

Mfanyibiashara Petro Porochenko, rais mteule wa Ukraine.
Mfanyibiashara Petro Porochenko, rais mteule wa Ukraine. DR

Tayari rais huyo mteule amejitokeza na kuahidi raia wa Ukraine kuwa atakomesha vita na kuleta amani nchini humo kutokana na mzozo wa kisiasa na usalama unaoendelea mashariki mwa nchi hio.

Poroshenko, amesema kitu cha kwanza kama rais atazuru mashariki mwa nchi hiyo kuhubiri amani.

Aidha amesema kuwa serikali yake haitatambua hatua ya Urusi ya kuchukua eneo la Crimea ambalo wakaazi wake miezi kadhaa iliyopita walipiga kura kujiunga na urusi.

Raia wa Ukraine zaidi ya milioni 30 walijitokeza kushirkki katika uchaguzi huo uliosusiwa na wakaazi wa mashariki mwa nchi hiyo likiwemo jimbo la Crimea.