POLAND-UKRAINE-Usalama-Diplomasia

Poland: Padri atekwa nyara mashariki mwa Ukraine

Waziri wa mambo ya kigeni wa Poland, Radoslaw Sikorski akielezea masikitiko yake juu ya kutekwa nyara kwa padri Pawel Witek, raia wa Poland.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Poland, Radoslaw Sikorski akielezea masikitiko yake juu ya kutekwa nyara kwa padri Pawel Witek, raia wa Poland. Reuters/Kacper Pempel

Kiongozi mmoja wa kidini raia wa Poland ametekwa nyara mashariki mwa Ukraine, waziri wa mambo ya kigeni wa Poland, Radoslaw Sikorski, amethibitisha.

Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo amebaini kwamba padri huyo ametekwa nya tangu jana na tayari jitihada za kumtafua zimeanza.

“Idara zetu za kibalozi zimeanza kumtafuta tangu jana, baada ya kutekwa nyara, na tunawasiliana viongozi wa kanisa”, amesema Sikorski katika mkutano na waandishi wa habari mjini Warsaw.

Sikorski amejizuia kutoa taarifa zaidi ili krahisisha jitihada za kupatikana kwa kiongozi huyo wa kidini.

Kwa mujibu wa vyombo vya Poland, padri Witek ametekwa nyara na waasi wa mashariki mwa Ukraine na kuziwiliwa katika makao makuu ya polisi ya Ukraine (SBU) mjini Donetsk, ambayo wanashikilia.