UKRAINE-URUSI-Usalama-Siasa

Ukraine: rais mpya aapa kukomesha machafuko mashariki

Rais wa Ukraine, Petro Porochenko, akionya wanaharakati wanaoshikiliwa maeneo ya mashariki mwa Ukraine.
Rais wa Ukraine, Petro Porochenko, akionya wanaharakati wanaoshikiliwa maeneo ya mashariki mwa Ukraine. REUTERS/David Mdzinarishvili

Rais mpya wa Ukraine Petro Porochenko ameahidi kukomesha mapigano mashjariki mwa Ukrane, ambako yanashuhudiwa machafuko baada ya wanaharakati wa eneo hilo kutangaza kuwa eneo lao limejitenga na Ukraine.

Matangazo ya kibiashara

Rais Petro Porochenko, ameyasema hayo katika mahojiano na gazeti la kila siku la Bild lililochapishwa jumatano wiki hii.

“Tumo katika hali ya vita mashariki mwa Ukraine, eneo la Crimea limeshikiliwa na Urusi na kuna hali ya usalama mdogo katika eneo hilo. Kwa hio tunapaswa kuonyesha msimamo wetu”, amesema Porochenko katika mahojiano hayo, ambayo alifanya akiwa pamoja na meya mtarajiwa wa mji wa Kiev, Vitali Klitschenko.

Rais huyo amebaini kwamba watahakikisha hali hio ya usalama mdogo inakomeshwa, huku akisema kwamba Urusi inachangia kwa kusababisha mdororo wa usalama mashariki mwa Ukraine.

Wapiganaji wakikijipanga kuanzisha mashambulizi karibu na uwanja wa ndege wa Donetsk, Ukraine, Mei 26 mwa 2014.
Wapiganaji wakikijipanga kuanzisha mashambulizi karibu na uwanja wa ndege wa Donetsk, Ukraine, Mei 26 mwa 2014. FP PHOTO / FABIO BUCCIARELLI

Akihojiwa iwapo ameamuru jeshi kuanzisha vita ili kurejesha eneo la mashariki mwa Ukraine linarejeshwa kwenye himaya ya utawala wa Ukraine, rais Porochenko, amejibu akisema kwamba hajatoa amri hio kwani bado hajakula kiapo ili awe rais rasmi wa taifa la Ukraine.

“Lakini hali halisia ni kwamba, ninawasiliana na serikali na nitaweza kusema kwamba operesheni dhidi ya ugaidi imeanza.

Porochenko ameonya kwamba kamwe hawataacha hali hio ya ugaidi hususan vitendo vya utekaji nyara na mauaji viendeleye, aidha kuendelea kufumbia macho tabia ya baadhi ya watu ya kushikilia au kudhibiti majengo ya serikali.

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel .
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel . REUTERS/Fabrizio Bensch

Kansela wa ujerumani Angela Merkel anatazamiwa kukutana kwa mazungumzo baada ya chakula cha jioni na waziri mkuu wa Ukraine, Arseni Iatseniouk, rais wa geogia Guiorgui Margvelachvili na rais wa Moldova Nicolae Timofti.