Raisi Poroshenko wa Urusi aapa kutokomeza wapiganaji wanaounga mkono Urusi
Imechapishwa:
Rais mteule wa Ukraine Petro Poroshenko amesema atapambana vilivyo na wapiganaji waliojihami na wanaoiunga mkono serikali ya Urusi, baada ya wapiganaji hao kudungua ndege ya jeshi na kusababisha vifo vya watu 14 akiwemo jenerali mmoja.
Udunguaji huo ulitekelezwa katika mji wa Sloviansk Mashariki mwa nchi hiyo, eneo ambalo limeeendelea kushuhudia machafuko kati ya wapiganaji hao na wanajeshi wa serikali ya Kiev.
Marekani inasema inasikitishwa na kuendelea kwa machafuko hayo ambayo inasema hii inaanisha kuwa wapiganaji hao wanapata usaidizi wa silaha kutoka nje ya nchi hiyo.
Jay Carney ni msemaji wa rais Barrack Obama.
Kaimu waziri wa ulinzi wa Ukraine Mykhailo Koval amesema ijumaa kuwa majeshi yamewasambaratisha baadhi ya maeneo ya mashariki ya Ukraine yaliyokuwa yametawaliwa na wanaharakati wanaounga mkono Urusi na kusababisha ukosefu wa usalama tangu mapema mwezi April.
Kiongozi huyo amenukuliwa akisema ''Jeshi letu limekamilisha operesheni dhidi ya wanaharakati huko magharibi mwa Ukraine Donetsk na sehemu ya kaskazini ya mkoa wa Lugansk " kaimu Waziri wa Ulinzi Mykhailo