Palestina

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameshutumu Hamas kutoka Mamlaka ya Palestina kuwateka vijana watatu raia wa Israel.

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu
Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu REUTERS/Gali Tibbon

Waziri Mkuu huyo wa Israel Benjamin Netanyahu amesisitiza kuwa Hamas ndio waliotekeleza utekaji nyara wa vijana watatu ambao ni wanafunzi raia wa Israel,walioripotiwa kukosekana katika ukingo wa magharibi karibu na Palestina wakati wakirejea nyumbani kutoka shuleni.Huku kundi la Hamas likikanusha kuhusika na utekaji huo.

Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya Waziri mkuu huyo wa Israel imethibitisha kuwa Netanyahu amekuwa na mazungumzo na rais wa mamlaka ya ndani ya Palestina Mahmoud Abbas hii leo siku ya jumatatu, na kumuahidia kusaidia katika juhudi za kuwatafuta vijana hao watatu wa Israel waliotoweka katika ukingo wa magharibi.

Mazungumzo hayo ya njia ya simu kati ya viongozi hao ni ya kwanza tangu Abbas kusaini makubaliano ya kuunda serikali ya muungano na kundi la Hamas mwezi Aprili na kusababisha Israel kusitisha mazungumzo ya amani na Wapalestina

Katika Hatua nyingine wanajeshi wa Israel nao wamemkamata spika wa bunge la Palestina Aziz Dweik ambaye pia ni mwanachama wa kundi la Hamas katika msako mkubwa wa kuwatafuta vijana hao, na kufanya idadi ya wapalestina waliokamatwa katika msako uliofanywa na jeshi la Israeli kufikia 150.

Uhusiano kati ya Isreal na Palestina ulidorora zaidi mwezi uliopita baada ya rais wa Palestina Mamhpoumd Abbbas kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa na kundi la Hamas ambalo Israeli inasema ni la kigaidi.