UJERUMANI-MAREKANI-Siasa-Diplomasia

Mkuu wa Idara ya ujasusi wa Marekani nchini Ujerumani atimuliwa

Rais wa Marekani Barack Obama.
Rais wa Marekani Barack Obama. Reuters/路透社

Serikali ya Ujerumani imemfukuza mkuu wa idara ya ujasusi wa Marekani nchini humo, uamuzi ambao huenda ukatikisa uhusiano wa kidplomasia kati ya Berlin na Washington DC. Afisa huyo anatuhumiwa kuhusika katika udukuzi wa mawasiliano ya sim ya viongozi wa serikali ya Ujerumani.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa zaidi zinasema kwamba hakuna ushahidi wowote unaoonyeshwa na Marekani kuhusu uwepo wa matukio ya udukuzi wa mawasiliano ya sim unadaiwa kutekelezwa na Marekani. Hatuwa iliyowaghabishwa viongozi wa Marekani na kuamuwa kuchukuwa uamuzi huo. Taarifa za serikali ya Ujerimani zinasema kwamba katika udukuzi huo mawasilinao ya sim ya Kansela Merkel pia yalichunguzwa.

Rais wa Marekani Barack Obama akiwa pamoja na kansela wa Ujerumani Angela Merkel.
Rais wa Marekani Barack Obama akiwa pamoja na kansela wa Ujerumani Angela Merkel. REUTERS/Kevin Lamarque

Ugunduzi katika siku za hivi karibuni, wa wapelelezi wawili wa Marekani katika idara ya ujasusi ya Ujerumani na kwenye wizara ya ulinzi, umepelekea Berlin kujibu kuchukuwa hatuwa ambayo ni nadra sana kuchukuliwa kwa mshirika wake wa karibu.

Mkuu wa upepelezi kwenye ubalozi wa Marekani jijini Berlin ametakiwa kuondoka nchini humo, huku Kansela Angela Merkel akisema kumfanyia udukuzi mshirika wake wa karibu ni kupoteza muda, kitendo ambacho waziri wake wa fedha Wolfgang Schäuble amekiita kuwa cha kijinga.

Vyombo vya habari nchini Ujerumani vimekua vikibaini kwamba uamzi wa kumfukuza mkuu wa idara ya upelelezi ya Mareakni nchini Ujerumani unaonyesha kudorora kwa uhusiano kati ya mataifa rafiki hayo.