MALAYSIA-UKRAINE

Mataifa ya magharibi yaitaka Urusi kushinikiza waasi mashariki mwa Ukraine kuruhusu kufikiwa kwa eneo la ajali ya ndege

Waangalizi wa kimataifa waliofika huko wamezuiwa na wapiganaji wanaounga mkono Urusi ambao wanadhibiti eneo la ajali.
Waangalizi wa kimataifa waliofika huko wamezuiwa na wapiganaji wanaounga mkono Urusi ambao wanadhibiti eneo la ajali. REUTERS/Maxim Zmeyev

Mataifa ya magharibi yameitaka Urusi kushinikiza waasi walioko Ukraine kuruhusu kufikiwa kwa eneo la ajali ya ndege ya Malaysia ya alhamisi.

Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte amesema amezungumza na raisi wa Urusi Vladimir Putin kuwa kiongozi huyo anao uwezo wa kusaidia na muda unakwenda na itakumbukwa kuwa waathirika wengi katika ajali hiyo walikuwa waholanzi.

Vilevile Marekani na Uingereza zimeiambia Urusi kuhakikisha eneo la tukio linafikika bila shida yoyote.

Waangalizi wa kimataifa waliofika huko wamezuiwa na wapiganaji wanaounga mkono Urusi ambao wanadhibiti eneo la ajali.

Pande zote mbili yaani waasi na serikali ya Ukraine zimerushiana lawama za kutekeleza mashambulizi dhidi ya ndege hiyo iliyokuwa ikifanya safari kutoka Armsterdam ikienlekea kuala lumpa ikiwa na takribani watu 298.