Pata taarifa kuu
UHOLANZI-UKRAINE-Usalama wa anga

Uholanzi : miili ya wahanga katika ajali ya MH17 yafikishwa Uholanzi

Jeneza ya mmoja ya wahanga waliyofariki katika ajali ya ndege yenye chapa MH17 ya Malaysia Airlines ikibebwa ndani ya ndege ili isafirishwe nchini Uholanzi, Julai 23 mwaka 2014.
Jeneza ya mmoja ya wahanga waliyofariki katika ajali ya ndege yenye chapa MH17 ya Malaysia Airlines ikibebwa ndani ya ndege ili isafirishwe nchini Uholanzi, Julai 23 mwaka 2014. REUTERS/Gleb Garanich
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Siku sita baada ya tukio, baadhi ya miili ya wahanga waliyofariki katika ajali ya ndege yenye chapa MH17 ya malaysia Airlines, imesafirishwa jumatano wiki hii nchini Uholanzi, ambako zoezi la kukagua miili ya wahanga itaanza. Kabla ya kusafirishwa miili hio ilichunguzwa na wataalam wa kimataifa nchini Ukraine.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa abiria ya 298 waliyokua ndani ya ndege hiyo, 193 ni raia wa Uholanzi, ambayo imetangaza jumatano wiki hii msiba wa kitaifa.

Miili ya watu hao imesafirishwa ikitokea katika mji wa Kharkiv, mashariki mwa Ukraine, mji ambao uko chini ya mamlaka ya serikali ya Ukraine. Mili arobaini ya wahanga hao imesafirishwa katika ndege mbili.

Serekali ya Kiev imeendelea kuinyooshea kidole Urusi kwamba inahusika na ajali hio ya ndege ya Malysia Airlines.

“Tutafanya kiliyo chini ya uwezo wetu ili kupata waliyohusika na tukio hilo, na kuwaadhibu kwa mujibu wa sheria. Sisi bado tunaona kwama Urusi ndiyo ilidungua ndege hiyo, naibu waziri wa Ukraine, Volodymyr Groïsman amesema kwenye uwanja wa ndege wakati alipokua akitoa heshima zake za mwisho kwa wahanga.

Mwakilishi wa ubalozi wa Uholanzi nchini Ukraine amepongeza juhudi za kusafirisha miili ya wahanga, ambao walikua ni wanawake , wanaume na watoto.

Wakaazi wa mji wa Kharkiv wamekua wakisubiri kwa heshima miili ya wahanga hao ,huko wengne wakija na shada za maua kutoa heshima zao za mwisho.

Hayo yakijiri, visanduku vya sauti vya ndege ya Malaysia Airlines vimefikishwa nchini Uingereza ili vifanyiwe uchunguzi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.