URUSI-UMOJA WA ULAYA-Vikwazo-Uchumi

Urusi: Putine ayachulia vikwazo mataiafa ya Ulaya

Rais wa Urusi, Vladimir Putine akiamuru kupigwa marufuku kuingia kwa bidhaa za Ulaya nchini Urusi.
Rais wa Urusi, Vladimir Putine akiamuru kupigwa marufuku kuingia kwa bidhaa za Ulaya nchini Urusi. REUTERS/Alexei Druzhinin/RIA Novosti/Kremlin

Baada ya mataifa ya Ulaya kuichukuliya Urusi vikwazo, hatimaye Urusi imeyachukulia mataifa hayo vikwazo katika sekta ya uchumi. Rais wa Urusi Vladimir Putine ameamuru jumatano wiki hii kupiga marufuku biashara ya bidhaa za kilimo kutoka Ulaya kuingia nchini Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Mpaka sasa, Kremlin imethibitisha kwamba vikwazop Urusi iliyochukuliwa na mataifa ya Ulaya haijaathiri sekata ya kilimo, na kuamuru kupiga vita bidha zote za kilimo kutoka mataifa ya Ulaya kuingia nchini Urusi.

Awali serikali ya Urusi kufuatia kudorora kwa hali ya afya, ilichukua vikwazo vya kutoingiza chini Urusi matunda na mbogamboga kutoka Poland, nyama kutoka Uholanzi au hata samaki kutoka Ugiriki. Lakini kwa sasa vikwazo hivyo vinalenga sekta ya kilimo kutoka mataifa yaliyoichukulia Urusi vikwazo hivi karibuni.

Poland imekua ikipata dola milioni 273 kwa matunda inayoingiza Urusi.
Poland imekua ikipata dola milioni 273 kwa matunda inayoingiza Urusi. REUTERS/Filip Klimaszewski

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Urusi, serikali itatoa orodha ya mataifa hayo al;hamisi wiki hii.. rias wa Urus Vladimir Putine amesema “ hatua hiyo imechukuliwa kwa lengo la kuimarisha usalama wa nchi na kulinda maslahi ya taifa.

Vikwazo hivyo vitadumu mwaka mmoja, lakini Kremlin imesema kuna uwezekano vikwazo hivyo virejelewe upya iwapo mataifa ya magharibi yatajirudi kwa vikwazo yaliyochukulia Urusi. Urusi imeanda mpango wa kushirikiana kibiashara na mataifa ya kusini mwa bara la Amerika.

Alhamisi wiki hii umeandaliwa mkutano kati ya mabalozi kutoa Ecuador, Brazil, Chile na Argentina. Mkutano huo utagubikwa na kupanda kwa bei za bidhaa kutoka mataifa hayo kwenye soka la Urusi.

Mataifa ya Ulaya yamebaini kwamba vikwazo hivyo vya Urusi havitaleta athari yoyote katika uchumi wao. Makampuni na mashirika 28 ya Ulaya yamekua yakiingiza bidhaa zao nchini Urusi, hususan katika sekta ya uchukuzi na kilimo.

Ulaya na Urusi vinategemeana kiuchumi. Urusi ni mshirika wa tatu katika sekta ya biashara na Ulaya. Iwapo Urusi itatekeleza uamzi wake wa kuyachukulia vikwazo mataifa ya Ulaya athari zitakua kubwa katika bara la Ulaya.

Mpaka sasa Umoja wa Ulaya umejizuia kutoa taarifa yoyote kuhusu vita hivyo vya kibiashara na Urusi, lakini wadadisi wanasema huenda mataifa ya Ulaya yakapoteza dola bilioni 40. Kwa hiyo bao ni mapema mno kuzungumzia hali hiyo.