UKRAINE-URUSI-EU-Vikwazo-Usalama

Mzozo mashariki mwa Ukraine unaendelea kutokota

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry (kushoto) pamoja na mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton (kulia), wakizungumzia kuhusu inavyoendelea nchini Ukraine. Ukraine, à Genève, le 17 avril 2014.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry (kushoto) pamoja na mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton (kulia), wakizungumzia kuhusu inavyoendelea nchini Ukraine. Ukraine, à Genève, le 17 avril 2014. REUTERS/Denis Balibouse

Timu inayofuatilia kwa karibu mzozo unaoendelea nchini Ukraine, ambayo inawajumuisha wajumbe wa Urusi, Ukraine pamoja na ujumbe wa jumuia ya usalama na maendeleo barani Ulaya, inaendelea na mazungumzo jumatatu wiki hii katika mji wa Minsk.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati ambapo kwa mara ya kwanza rais wa Urusi ametangaza kutambuliwa kama taifa huru eneo la mashariki mwa Ukraine linalodhibitiwa na waasi.

Hata hivo mapigano bado yanaendelea kushuhudiwa mashariki mwa Ukraine kati ya jeshi la serikali na waasi waliojitenga na Kiev, huku waasi hao wakiendelea kutwaa baadhi ya maeneo, na kutangaza kuendelea na mashambulizi dhi ya jeshi hilo la Ukraine.

Rais wa Urusi, vladimir Putin.
Rais wa Urusi, vladimir Putin. Reuters/路透社

Tangazo hilo la rais wa Urusi, Vladimir Putin limezua tafrani siku mbili baada ya mkutano wa Umoja wa Ulaya uliyoipa Urusi muda wa wiki moja ili iwe imesitisha kuwasaidia kijeshi waasi wa mashariki mwa Ukraine kwa kuepuka vikwazo.

Halmashauri ya Umoja wa Ulaya ilipewa hivi karibuni jukumu la kuandaa haraka iwezekanavyo tangu jumatatu wiki hii vikwazo dhidi ya Urusi, na kuviwasilisha mwishoni mwa wiki hii kwa viongozi wa Umoja wa Ulaya, ambao wataichukulia vikwazo Urusi kulingana na jinsi hali inavyoendelea nchini Ukraine.

Umoja wa Ulaya umetupilia mbali uwezekano wa kuipa silaha serikali ya Kiev, baada ya baadhi ya marais wa mataifa ya Ulaya ya mashariki na maseneta wa Marekani kupendekeza Ukraine isaidiwe kijeshi.

Hata hivo Marekani imekataa uwezekano wa kuingilia kijeshi Ukraine kama suluhu la mgogoro unaoendelea.