UINGEREZA-ISIL-Haki za binadam

Uingereza yatiwa hofu na hali inayomkabili raia wake anaeshikiliwa mateka

Serikali ya Uingereza imeelezea wasiwasi wake juu ya mateka raia wa taifa kilo anaeshikiliwa na wapiganaji wa Kiislam, ambaye wapiganaji hao wamesema katika mkanda waliyorusha kwenye mitandao yao kwamba atauawa hivi karibuni.

David Cameron, waziri mkuu wa Uingereza.
David Cameron, waziri mkuu wa Uingereza. REUTERS/Olivia Harris
Matangazo ya kibiashara

Baada ya taarifa ya kuuwawa kwa mwanahabari wa pili raia wa Marekani na wapiganaji wa kiislam, waziri mkuu wa Uingereza David Cameron ameitisha mapema jumatano asubuhi kikao cha dharura cha baraza la mawaziri ili kujadili taarifa hiyo ya wapiganaji wa kiislam.

Davi cameron amekua wa kwanza kutoa msimamo wake kuhusu mauaji ya mwanahabari wa pili , ambaye ni raia wa Marekani, baada ya wapiganaji wa kiisla kutoa mkanda wa mauaji hayo na kukiri kwamba wao ndio wamehusika na mauaji hayo. Waziri mkuu wa Uingereza maelani mauaji hayo na kusema kwamba ni kitendo cha kikatili.

Mkanda huu uliyorushwa na wapiganaji wa kiislam unaitia hofu serikali ya Uingereza, hata kama serikali hiyo ilikua bado haijawahi kutangaza rasmi kwamba kuna raia wa Uingereza anaeshikiliwa mateka na wapiganaji wa kiislamu.

Hata hivo wizara ya mambo ya nje ya Uingereza iliwahi kuwataka wanahabari kutotoa taarifa yoyote kuhusu kuwepo kwa raia wa Uingereza anaeshikiliwa mateka na wapiganaji wa kiislam.

Mkanda huo mpya uliyorushwa hewani, umepelekea serikali ya Uingereza kutangaza kuwepo kwa raia wake anaeshikiliwa mateka na wapiganaji wa kiislam, ambao wamesema kuwa ndiye atakaefuatiwa kwa kukatwa kichwa.