NATO-UKRAINE-URUSI-ISIL-Usalama

Mkutano wa viongozi wa mataifa wanachama wa NATO waanza

Marais na viongozi wa serikali zaidi ya sitini kutoka mataifa wanachama wa jumuiya ya kujihami ya mataifa ya magharibi NATO, wanakutana tangu alhamisi wiki hii kwa muda wa siku mbili.

Mvutano kati ya Ukraine na Urusi na harakati za wapiganaji wa kiislam, ni masuala tete yatakayogubika mkutano wa NATO unaoanza alhamisi, Septemba 4 mwaka 2014.
Mvutano kati ya Ukraine na Urusi na harakati za wapiganaji wa kiislam, ni masuala tete yatakayogubika mkutano wa NATO unaoanza alhamisi, Septemba 4 mwaka 2014. REUTERS/Leon Neal/Pool
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wanaoshiriki mkutano huo wa kilele unaofanyika katika mji wa Newport, nchini Wales wanatazamia kujadili migogoro inayojitokeza katika mataifa mbalimbali duniani, hususan mvutano kati ya Urusi na Ukraine.

Katika mkutano huu wa siku mbili, viongozi hao watajaribu kusema kwa sauti moja kwa rais wa Urusi Vladimir Putin, ambaye nchi yake inatuhumiwa kuhusika moja kwa moja katika vita nchini Ukraine, kwa kumtumia ujumbe wa kujirekebisha.

Rais Barack Obama alifahamisha jumatano wiki hii kufanya ziara katika nchi ya Wales ambapo alipanga kukutana na marais wa Estonia, Latvia na Lithuania, ambazo zamani ziliokua washirika wa karibu wa Urusi, na kwa sasa ni nchi wanachama wa NATO, ili kuwapa moyo na kuionya Urusi. "Ni lazima Ukraine iungwe mkono", Barack Obama amesema alhamisi wiki hii.

Uamuzi wa Ufaransa wa kusitisha utoaji wa meli ya kivita ya Mistral kwa Urusi umeribishwa na washirika katika mkutano huo.

Hata hivo Ukraine si mwanachama wa NATO, lakini mataifa wanachama wa jumuiya hiyo wamekubali kuitolea msaada wa Uro milioni 12 ili iweze kuimarisha jeshi lake.

Suala jingine tete litakalo zungumziwa katika mkutano huo ni pamoja na tishio la serikali ya Kiislamu. Tayari Washington imetoa wito wa wa kushirikiana kwa pamoja ili kuweka mkakati thabiti dhidi ya wapiganaji wa kiislam.