Ufaransa: manowari za kivita za Urusi zazuiliwa
Imechapishwa: Imehaririwa:
Ufaransa imeamua kuongeza shinikizo juu ya Moscow la kuzuia manowari mbili za kivita Mistral zilizonunuliwa na Urusi.
Moscow imekua ikijaribu kupuuzia ujumbe huu, ambao huenda ukasababisha madhara makubwa katika sekta ya uchumi nchini Ufaransa.
Uamzi huo unachukuliwa baada ya rais wa Urusi, Vladimir Putin, kutoa tangazo jumatano wiki hii la mpango wa kukomesha mgogoro mashariki mwa Ukraine.
Ufaransa imekua ikipata shinikizo kutoka mataifa ya Ulaya, nchi za Baltics, Ukraine na mataifa wanachama wa NATO. Hatimaye Paris imetangaza kusimamisha mpango huo wa mauzo ya Manowari, wakati moja ya manowari hizo ingelisafirishwa nchini Urusi mwezi Oktoba."Pamoja na matarajio ya kusitisha mapigano na kutekelezwa moja kwa moja, kuna utaratibu ambao haujakaa sawa ili Ufaransa iruhusu kusafirishwa kwa manowari hizo” ikulu ya Paris imesema katika tangazo lake.
Kusitishwa kwa kusafirishwa kwa manowari hizo haimaanishi kwamba hazitosafirishwa, bali ni njia moja wapo ya Ufaransa kuepuka lawama katika mkutano unaozishirikisha nchi wanachama wa TANO, ambao umeanza alhamisi wiki hii. Hii pia ni njia mbadala wa kuishawishi Urusi kuchangia kuleta amani nchini Ukraine.
Urusi imeilaumu Ufaransa kwa uamuzi huo ikibaini kwamba Ufaransa imekua ikipata vishawishi kutoka Marekani. Wakati huo huo, waziri wa ulinzi wa Urusi, amesema kwamba jeshi la Urusi halitoathirika kutokana na hatua hiyo ya Ufaransa.