URUSI-UKRAINE

Huenda muafaka ukapatikana baina ya Ukraine na waasi

Baada ya mzozo wa miezi kadhaa huko mashariki mwa Ukraine, marais wa Urusi Vladimir Poutine na yule wa Ukraine Petro Porochenko wanaelekea kumaliza mzozo huo wakati huu mazungumzo yamepangwa kufanyika hi leo na huenda makubaliano ya kusitisha vita yakafikiwa licha ya madai kutoka Urusi, Ukraine na upande wa waasi kutofautiana.

Kramatorsk, 02/09/2014
Kramatorsk, 02/09/2014 REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ukraine Petro Porochenko amefahamisha hapo jana kwamba ataamuru majeshi yake kusitisha vita iwapo mazungumzo yataanzishwa baina ya wawakilishi wa serikali yake, na ile ya Urusi pamoja na wawakilishi wa baraza la Usalama la Ulaya wakishirikishwa pia waasi wa kaskazini mwa Ukraine yanatarajiwa kuzindinduliwa hii leo huko Misnk.

Waasi wa Ukraine nao upande wao wameahidi pia kusitisha vita hii leo Ijumaa saa tisa majira ya kimataifa katika miji ya Donetsk na Loungansk iwapo makubaliano yatafikiwa au tu pale serikali ya Ukraine itasaini mpango wa kutatuwa matatizo kwa nji aya kisiasa.

Upande wa Ukraine, wanaona kuwa swala la usitishwaji mapigano ni changamoto kubwa. lakini serikali ya kiev yasema ipo tayari kukabiliana na changamoto hiyo huku ikitowa masharti yake. moja miongoni mwa masharti yake ni pamoja na mpaka wa Urusi na Ukraine kulindwa taasisi ya usalama na ushirikiano katika bara la Ulaya, na majeshi ya Urusi yaliotumwa Ukraine kuondoka nchini humo, huku Urusi na waasi wakitakiwa kuwaachia huru wanajeshi wa Ukraine waliotekwa.

Upande wa Urusi, Vladimiri Poutine anatofautiana kabisa na hayo, kwanza anapinga kabisa kuihusisha nchi yake na mzozo wa Ukraine na waasi na anaendelea kuitolea wito serikali ya Ukraine kusitisha mashambulizi yake ya anga katika maeneo ya raia mashariki mwa Ukraine

kumekuwa na wasiwasi ya kufikia muafaka kutokana na mitazamo tofauti iliopo baina ya pande husika na mzozo huo, lakinik katika mvutano huo wa kidiplomasia Urusi inaonekana kuchukuwa nafasi. kwenye uwanja wa mapambano, kutekwa kwa miji iliokuwa chini ya umiliki wa serikali kumeidhoofisha serikali ya kiev na kuiweka katika hali mbaya na kumfanya rais Porochenko kuonekana kuwa dhaifu mbele ya Vladimir Poutine

Wakati huo huo viongozi wa nchi za Jumuiya ya Kujihami ya nchi za Magharibi Nato, wameendelea kusisitiza uungwaji wao mkono kwa viongozi wa Ukraine bila hata hivyo kutowa msaada wa silaha lakini kuliwezesha jeshi kwa kulipa vifaa vya kisasa lakini pia kutowa matibabu kwa wanajeshi wataojeruhiwa katika mapigano kwa kitita kinacholingana na Euro milioni 15 ambazo zitaongezwa katika misaada kati ya pande mbili ya nchi wanachama wa Nato wataohitaji kutowa msaada.

Mbali na hayo Nato imesisitiza kuhusu uungwaji wake mkono kwa Ukraine huku ikikosoa hatuwa ya Urusi kuingiza majeshi katika ardhi ya Ukraine.

wakati huo huo viongozi wa Ulaya na Marekani wanaelekea kuiwekea Urusi vikwazo zaidi katika kuendelea kumshinikiza rais Poutine kutoendelea kuwaunga mkono waasi wanaopambana na serikali ya Kiev sambsyo kwa sasa yaoenekana kuelemewa na waasi.