Ukraine: mapigano yaendelea
Imechapishwa: Imehaririwa:
Mashambulizi mapya yametokea usiku wa jumapili kuamkia jumatatu wiki hii karibu na mji wa mwambao wa Marioupol, mashariki mwa Ukraine. Milio ya risase inaendelea kusikika na kupelekea makubaliano yakusitisha mapigano kuwa hatarini.
Miliyo ya zana nzitonzito inaendela kusikika mashariki mwa Ukraine. Kundi moja la raia wa Ukraine waliyojitoa muhanga kwa kupigania uhuru wa Ukraine wameshambuliwa kwa bomu jumapili mwishoni mwa juma liliyopita kwenye moja ya ngome yao katika mji wa Marioupol, huku milipuko ya mabomu ikiendelea kusikika usiku mzima wa jumapili.
Hali ya wasiwasi imeendelea kutanda nchini Ukraine, licha ya viongozi wa Urusi na Ukraine kusaini makubaliano ya kusitisha mapigano mashariki mwa Ukraine.
Katika mazungumzo ya simu pamoja na kansela wa Ujerumani, Angela Markel, rais wa Ukraine Petro Porochenko amejizuia kusema kinachoendelea mashariki mwa Ukraine, huku akiendelea kupongeza juhudi za kusaini makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Urusi na Ukraine mjini Minsk.
Rais porochenko amaekua na imani ya kutuma tume ya waangalizi wa jumuiya ya usalama na maendeleo barani Ulaya kwenye eneo kunakoshuhudiwa mapigano, huku akiwa na imani kwamba masharti ya kusitisha mapigano yatakua yametekelezwa kabla ya kuunza kwa mazungumzo kati ya pande zinazo husika katika machafuko hayo.
Viongozi wa waasi wa Ukraine wamependekeza kuongezwa kwa ibara ya kuutambua uhuru wa maeneo yanayothibitiwa na waasi kwenye makubailiano ya kusitisha mapigano yaliyosainiwa mjini Minsk.
Wakati huo huo, waziri mkuu wa Ukraine, Arseni Iatseniouk ametangaza kwamba iwapo makubaliano hayo yataambulia patupu, huenda akaomba sheria ya kijeshi iwekwe katika eneo la mashariki mwa Ukraine.