David Cameron alaani mauaji ya Muingereza David Haines

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron ajiapiza kukabiliana na wauaji nchini Iraq
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron ajiapiza kukabiliana na wauaji nchini Iraq REUTERS

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amelaani mauaji ya kikatili yaliyofanywa kwa mfanyakazi wa misaada David Haines baada ya kutolewa kwa video ya wapiganaji wa dola ya kiislamu hapo jana inayoonyesha kichwa cha mateka huyo raia wa Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Bwana Cameroon amejiapiza kufanya kufanya kila liwezekanalo ili kuwasaka na kuwabaini wauaji na anayefadhili ukatili huo.

Video ya hivi Karibuni ilikuwa pia na tishio la kumuua mateka wapili ambaye ni raia wa Uingereza.

Rais wa Marekani Barack Obama ameguswa na kuungana na uingereza katika huzuni wakati huu David Cameron akikabiliwa wito wa kuruhusu majeshi ya uingereza kusaidia mpango wa washngton kukabiliana na kundi hilo la kigaidi linalosambaa.

Waziri wa mkuu wa Uingereza ataongoza kikao cha dharura cha kamati ya cobra mapema hii leo kujadili hatua za kuchukua baada ya video ya IS kuonesha mpiganaji wake aliyeficha sura yake akimuua mateka raia wa Uingereza.

Wapiganaji wa dola la kiislamu tayari wameua kwa kukata vichwa Wamarekani wawili, kwa kusema ilikuwa katika kukabiliana na Marekani ambayo imekuwa ikifanya mashambulizi ya anga nchini Iraq.