UFARANSA-ISLAMIC STATE-Usalama-Diplomasia

Ufaransa: Mkutano uhusuo amani na usalama nchini Iraq

Rais wa Ufaransa, François Hollande, akimpokea rais wa Iraq Fouad Mansoum katika Ikulu ya Elysée, ukuisubiriwa mkutano uhusuo amani na usalama nchini Iraq.
Rais wa Ufaransa, François Hollande, akimpokea rais wa Iraq Fouad Mansoum katika Ikulu ya Elysée, ukuisubiriwa mkutano uhusuo amani na usalama nchini Iraq. REUTERS/John Schults

Viongozi wa mataifa mbalimbali wanataraji kukutana jumatatu wiki hii jijini paris nchini Ufaransa, katika mkutano uhusuo usalama nchini Iraq na kupanga mbinu za kutumia katika kulipiga vita kundi la Islamic State ambalo limetangaza kumkata kichwa mateka mwingine wa Uingereza David Haines mfanyakazi wa mashirika ya kimisaada.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo unalenga kutowa jukumu kwa kila nchi iliojiunga katika muungano wa kimataifa ulioanzishwa na Marekani juu ya kupanga mikakati ya kupambana na kundi la Islamic State. Rais wa Ufaransa François Hollande anataraji kuhutubia katika uzinduzi wa mkutano huo utaohudhuriwa na takriban ma rais zaidi 20.

Hayo yanajiri wakati Marekani ikitangaza kupata uungwaji mkono wa nchi 40 zitazojiunga katika muungano wa kimataifa juu ya kupambana na kundi la Islamic State IS. Kati ya nchi hizo 40, 25 pekee ndizo zilizo tajwa bayana huku nyingine zikijizuia kutajwa kutokana na sababu za kuvuruga mpango mzima.

Serikali ya Iran ambayo haikupewa mualiko wa kushiriki katika mkutano huo, imesema haina haja ya kuhudhuria. Serikali ya Iran imekuwa katika mstari wa mbele kutowa uwezo na ushauri wa kijeshi kwa serikali ya wapiganaji wa kikurdi wanaopambana na wapiganaji wa Islamic State wakati huu Iran ikikataa kushiriki katika muungano huo unaoongozwa na Marekani, huku serikali ya Washington ikitupilia mbali ushirikiano wowote na Iran.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amekuwa katika mstari wa mbele kuzishawishi Misri ambayo imetowa masharti ya muungano huo kuwa chini ya kivuli cha Umoja wa Mataifa pamoja na Uturuki ambayo hadi sasa imepinga kushiriki katika operesheni za kijeshi.

Canada imekubali kutowa wanajeshi wake wataojiunga na jeshi la Marekani, Ufaransa yao imetowa uwezo wa kijeshi kwa wapiganaji wa kikurdi, na takriban tani 58 ya nafaka za chakula kama msaada wa kibinadamu katika mji wa Arbil.

Wakati huo huo serikali ya Uingereza imeongeza uwezo zaidi ya silaha kwa wapiganani wa kikurdi huku ikikubali kushiriki katika operesheni ya mashambulizi ya anga, huku Australia ikikubali kutuma wanajeshi 600 nchini Saudia Arabia kujiunga na muungano huo.