UINGEREZA-SCOTLAND-Siasa-Kura ya maoni

Uingereza: saa chache kabla ya kura ya maoni Scotland

Wakati kukisubiriwa kura ya maoni kuamua Scotland kuwa huru alhamisi wiki hii, takwimu zinaonyesha kuwa kura ya hapana inaongoza kwa asilimia chache dhidi ya kura ya ndio huku shikinizo zaidi ikiendelea kuhakikisha kura ya hapana inashinda.

Kura ya maoni kuhusu ndio au hapana kwa kujitawala kwa Scotland inasubiriwa alhamisi sepemba 18 mwaka 2014.
Kura ya maoni kuhusu ndio au hapana kwa kujitawala kwa Scotland inasubiriwa alhamisi sepemba 18 mwaka 2014. REUTERS/Paul Hackett
Matangazo ya kibiashara

Harakati zaendelea kwenye mitandao ya kijamii nchini Uingereza na Scotland kuhusu kura ya maoni ya kujitawala kwa Scotland au la.. 
Harakati zaendelea kwenye mitandao ya kijamii nchini Uingereza na Scotland kuhusu kura ya maoni ya kujitawala kwa Scotland au la..  DR

Takwimu hizo zinaonyesha kura ya hapana inaongoza kwa asilimia 52 dhidi ya 48 ya hapana. Takwimu hizi zilizo fanyika kwa nyakati tofauti zimeonesha mvutano kati ya wale wanaotaka Uhuru wa Scotland na wale wanaopinga eneo hilo kujitenga na Uingereza.

Kiongozi wa uguvugu linalo taka mjitengo Blair Jenkions amesema kuridhishwa na kiwango hicho ambacho anaona kura ya ndio itashinda na hivo eneo hilo kuwa huru.

Jumanne wiki hiii vyama vikuu vitatu nchini Uingereza vimetowa ahadi kwa wananchi wa Scotland iwapo kura ya hapana itashinda, watatowa uwezo zaidi kwa bunge na kujitegemea.

Kulingana na ahadi hizo, iwapo kura ya hapana itashinda, majadiliano ya kutowa madaraka kwa utawala mpya yatanzishwa punde tu baada ya kura hiyo ya maoni, lakini pia serikali ya Scotland ndio itakuwa na kauli ya mwisho katika kuchukuwa maamuzi kuhusu swala la fedha.

Upande wake waziri mkuu wa Scotland na bingwa wa kutetea kura ya ndio, Alex Salmond, amesema hii itakuwa ni fursa muhimu kwa wananchi wa Scontland wanaotakiwa kuitumia kwa kupiga kura ya ndio ili nchi hiyo ijitawale.