UINGEREZA-SCOTLAND-Siasa-Kura ya maoni

Scotland: raia wanaounga mkono uhuru wameapa kupambana hadi mwisho

Mwanamke huyu anashikilia bendera ya Scotland wakati wa mkutano wa raia wanaounga mkono uhuru wa Scotland
Mwanamke huyu anashikilia bendera ya Scotland wakati wa mkutano wa raia wanaounga mkono uhuru wa Scotland REUTERS/Dylan Martinez

“ Ndio” au “ hapana” kwa uhuru wa Scotland. Jibu linasubiriwa ijumaa wiki hii Septemba. Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa tangu saa kumi na mbili asubuhi alhamisi wiki hii saa za kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Maelfu kwa mamia ya wapiga kura wametakiwa kupiga kura, na wengi wao hawajajua watakua upande gani kwa kupiga kura.

Katika maeneo mengi “ ndio” inatawala : “ yes”ikimaanisha “ndio” imeandikwa sehemu nyingi, hususan barabarani kwenye kuta za nyumba kwenye kofia na sehemu zingine, ikimaanisha kuwa wanaunga mkono Scotland iwe huru. “ Hapana” inaonekana kwa uchache, hususan kwenye madirisha na miliango. Raiua wanaounga mkono uhuru wa Scotland wamekua wakifanya kampeni ya kuhimiza raia kupiga kura ya “ ndi” kwa uhuru wa Scottland.

Jumanne takwimu zilionesha kuwa kura ya “ hapana” inaongoza kwa asilimia chache dhidi ya kura ya “ ndio” huku shikinizo zaidi ikiendelea kuhakikisha kura ya hapana inashinda.

Takwimu hizo zilionesha kura ya hapana inaongoza kwa asilimia 52 dhidi ya 48 ya hapana. Takwimu hizi zilizo fanyika kwa nyakati tofauti zilionesha mvutano kati ya wale wanaotaka Uhuru wa Scotland na wale wanaopinga eneo hilo kujitenga na Uingereza.
Kiongozi wa uguvugu linalo taka mjitengo Blair Jenkions amesema kuridhishwa na kiwango hicho ambacho anaona kura ya ndio itashinda na hivo eneo hilo kuwa huru.