UINGEREZA-SCOTLAND-Siasa-Kura ya maoni

Scotland yasalia eneo la Uingereza

Alhamisi wiki hii watu milioni nne wa Scotland wameonesha misimamo yao kuhusu kujitenga au kusalia chini ya utawala wa Uingereza, swali ambalo ambalo kwa sasa limepatiwa ufumbuzi.

Kundi la watu wanaonga mkono Scotland kusalia chini ya utawala wa Uingereza wakidhihirisha furaha yao.
Kundi la watu wanaonga mkono Scotland kusalia chini ya utawala wa Uingereza wakidhihirisha furaha yao. REUTERS/Dylan Martinez
Matangazo ya kibiashara

Kura ya “ hapana” imeshinda kwa asilimia 55.3, na kuamua Scotland iendeleye kuwa chini ya utawala wa uingereza.

Kwa sasa zoezi la uhesabuji kura imefikia tamati, huku kundi la watu wanaounga mkono Scotland kuendelea kusalia chini ya uongozi wa Uingereza wakidhihirisha furaha yao. Kura ya “ hapana” inaongoza kwa asilimia 55.3 dhidi ya kura ya “ ndio” ambayo ni asilimia 44.70

Hata hivo waziri mkuu wa Scotland, Alex Salmon, amekubali kushindwa licha ya harakati zake za kutetea uhuru wa Scotland kugonga mwamba. Lakini ameiomba serikali ya Uingereza kuheshimu haraka iwezekanavyo ahadi zake kwa kukabidhi raia wa Scotland kujitawala.

Wakati huo huo waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, amempongeza kiongozi wa kundi la watu wanauunga mkono muungano, Alistair Darling, kwa “ kampeni alizoendesha dhidi ya kujitenga kwa Scotland”.

Kura hizo zimekua zikitofautiana kulingana na miji au mikoa. Katika mji wa Edimbourg, kura ya “ hapana” imeongoza, tofauti na mji wenye watu wengi wa Scotland, Glasgow. Katika mji wa tatu kwa ukubwa, Aberdeen, kura ya “ hapana” imefikia asilimia 58,6.