UFARANSA-ISLAMIC STATE-Usalama-Diplomasia

Ufaransa yashambulia Dola la kiislam

Aina ya  ndege ziliyoendesha mashambulizi dhidi ya ngome za wapiganaji wa Dola la Kiislam, ijumaa Desemba 19 mwaka 2014.
Aina ya ndege ziliyoendesha mashambulizi dhidi ya ngome za wapiganaji wa Dola la Kiislam, ijumaa Desemba 19 mwaka 2014. Dassault Aviation

Ikulu ya Ufaransa imetangaza ijuma wiki hii kwamba ndege zake za kijeshi zimeshambulia kwa mara ya kwanza ngome za wapiganaji wa Dola la Kiislam kaskazini mashariki mwa Iraq.

Matangazo ya kibiashara

Ufaransa inashiriki katika vita vingine dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam nchini Iraq na Syria, baada ya kutuma wanajeshi wake nchini Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Ufaransa ni taifa la pili lenye nguvu duniani kuingia katika vita nchini Iraq, ikiiunga mkono Marekani katika vita vyake dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Tangazo hilo la Ikulu ya Paris limebaini kwamba mashambulizi ya kwanza yameendeshwa katika baadhi ya maeneo mapema ijumaa wiki hii. Ndege za kijeshi zimekua zikilenga ngome za wapiganaji wa Dola la Kiislam kaskazini mashariki mwa Iraq.

Tangazo hilo limethibitisha kwamba ghala la vifaa vya kijeshi vya wapiganaji wa Dola la Kiislam limeteketezwa na mashambulizi hayo, huku likibaini kwamba mashambulizi hayo yataendelea hivi karibuni. Ndege hizo ziliyoendesha mashambulizi hayo zimerejea kwenye vitu vyao viliyotengwa katika mji wa Abou Dhabi kwenye umbali wa kilomita 1500 na eneo lililoshambuliwa.

Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi, operesheni dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam imeendeshwa katika jimbo la Mossoul, nchini Iraq. Mashambulizi hayo yameendeshwa na ndege mbili za kijeshi ambazo zimekua zimebeba mabomu aina ya GBU 12, na aina nyingine ya ndege yenye chapa C-135FR pamoja na ndege nyingine ambayo imekua ikisaidia kupiga doria kwenye bahari Atlantic 2.

Mashambulizi hayo ya anga yametekelezwa chini ya uongozi wa jeshi la Ufaransa kwa ushirikiano na viongozi wa Iraq pamoja na washirika wa Ufaransa katika jimbo hilo, wizara ya ulinzi imebaini .

Alhamisi wiki hii katika mkutano na waandishi wa habari, rais wa Ufaransa François Hollande, alibaini kwamba muda umewadia wa kuanzisha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam.