UINGEREZA-SCOTLAND-Siasa-Kura ya maoni

Uingereza: Scotland: kura ya “ hapana” inaongoza

Raia wa Scotland wanauunga mkono muungano wa Uingereza wakifurahia ushindi dhidi ya Uhuru wa Scotland.
Raia wa Scotland wanauunga mkono muungano wa Uingereza wakifurahia ushindi dhidi ya Uhuru wa Scotland. REUTERS/Dylan Martinez

Matokeo ya awali ya kura ya maoni nchini Scotland yameanza kutolewa mapema ijuma asubuhi baada ya kura iliopigwa alhamisi wiki hii, huku asilimia 92 ya wananchi wa Uingereza wakiendelea kusubiri matokeo rasmi ya uchaguzi huo wa kihistoria.

Matangazo ya kibiashara

Matokeo hayo ya awali yanaonyesha kuwa kura ya hapana kupinga eneo hilo kujitenga na Uingereza ndio inaongoza kwa asilimia 58.

Wananchi wanaokadiriwa kati ya asilimia 80 na 90 ndio waliohudhiria uchaguzi huu, sawa na watu zaidi ya milioni 4 wa nchi hiyo. Alhamisi wiki hii kwenye mitandao ya kijamii inayongozwa na mchezaji wa Tenis, Andy Murray, mwenye asili ya Scotland aliendelea kutowa wito wa kupiga kura ya ndio eneo hilo kujitenga na Uingereza.

Hata hivo waziri mkuu wa Scotland, Alex Salmon, amekubali kushindwa licha ya harakati zake za kutetea uhuru wa Scotland kugonga mwamba. Lakini ameiomba serikali ya Uingereza kuheshimu haraka iwezekanavyo ahadi zake kwa kukabidhi raia wa Scotland kujitawala.

Wakati huo huo waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, amempongeza kiongozi wa kundi la watu wanauunga mkono muungano, Alistair Darling, kwa “ kampeni alizoendesha dhidi ya kujitenga kwa Scotland”.

Kura hizo zimekua zikitofautiana kulingana na miji au mikoa. Katika mji wa Edimbourg, kura ya “ hapana” imeongoza, tofauti na mji wenye watu wengi wa Scotland, Glasgow. Katika mji wa tatu kwa ukubwa, Aberdeen, kura ya “ hapana” imefikia asilimia 58,6.