UFARANSA-ISLAMIC STATE-Usalama-Diplomasia

François Hollande aapa kutokomeza IS

katika mkutano wa Umoja wa Mataifa, François Hollande anatazamiwa kutoa tangazo kuhusu hatma ya mateka wa Ufaransa anaeshikiliwa Algeria.
katika mkutano wa Umoja wa Mataifa, François Hollande anatazamiwa kutoa tangazo kuhusu hatma ya mateka wa Ufaransa anaeshikiliwa Algeria. REUTERS/Alain Jocard

Rais wa Ufaransa François Hollande ambaye anashiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini New York ameonekana kuwa na hofu ya mapambano dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam pamoja na hatma ya mateka wa Ufaransa, Hervé Gourdel, anaeshikiliwa Algeria.

Matangazo ya kibiashara

Hatima ya mateka huyo wa Ufaransa nchini Algeria ni suala mtambuka ambalo linaonekana kutokumpa rais Hollande utulivu mjini New York, akionekana kujali hali ya familia ya Hervé Gourdel, hata kwa kuwapigia simu, kuwasaliana mara kwa mara na viongozi wenzake mjini Paris wakiwemo mawaziri wake wa Ulinzi na wa Mambo ya ndani.

Kuhusiana na hatua ya ushirikiano katika mapambano dhidi ya Dola la Kiislamu, nchi ya Ufaransa iko katika mstari wa mbele ukizingatia kauli nzito zinazoashiria nchi yake kujikita kwenye vita vya muda mrefu, vita hivi vikiwa vya tatu tangu ashike madaraka, baada ya operesheni Serval nchini Mali na operesheni Sangaris nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
“ Tuko katika vita, ambavyo vitadumu muda mrefu”, amesema rais Hollande.

Katika azma ya nchi ya Ufaransa kuepuka kuonekana kushika mkia kama inavyokosolewa mara kadhaa katika kushirikiana na Marekani, rais Hollande ameonekana kutetea mgawanyo wamajukumu baina ya nchi yake na Marekani, hasa kwa kujikita katika kusaka suluhu kwa njia ya kisiasa sambamba na ya kijeshi.

Siku ya Jumanne wiki hii, rais François Hollande amekutana na mwenzake wa Iran kama mwaka uliopita, na hii itakuwa mara ya kwanza katika miaka kadhaa iliyopita kwa nchi ya Iran kushirikiana na nchi za Magharibi, lengo likiwa kulitokomeza kundi la Dola la Kiislamu ambalo bila shaka hatma yake itajadiliwa kwa kina katika Mkutano Mkuu wa 69 Umoja wa Mataifa unaotarajiwa kuanza rasmi leo jumatano.