Ukraine - Urusi

Mkataba wa kusitisha vita wavunjwa nchini Ukraine watu 3 wauawa

Watu watatu wamepoteza maisha na wengine watano wamejeruhiwa jana jumapili katika mji wa Donetsk, kitovu cha waasi wanaoipinga serikali ya Ukraine, licha ya ukimya wa milio ya risase kati ya wanajeshi na wapiganaji wanaodai mjitengo na Ukraine.

Ubadilishanaji wafungwa eneo la mashariki mwa Donetsk, Septemba 28.
Ubadilishanaji wafungwa eneo la mashariki mwa Donetsk, Septemba 28. REUTERS/Marko Djurica
Matangazo ya kibiashara

Majadiliano ya kutafuta muafaka katika mgogoro wa Ukraine yanaendelea, yakiwa na lengo la kuhakikisha pande zote mbili zinasitisha mashambulizi na hakuna milio ya risase itayo sikika tena kutoka pande zote mbili, wakati huu kukisubiriwa kuondoka kwa vikosi vya pande zote mbili kwenye uwanja wa mapambano na kukaa kwenye umbali wa kilometa 30.

Vikosi vya Ukraine vinasubiri kuona makundi ya waasi yanaondoka katika maeneo mbalimbali waliokubaliana na kujiweka kando kwenye umbali wa kilometa 30 eneo la mashariki. Msemaji wa jeshi la Ukraine Andriy Lysenko amesema kuna hatuwa zilizopigwa hadi sasa wakati huu ubadilishanani wa wafungwa ukifanyika jana jumapili Septemba 28.

Licha ya hatuwa kubwa zilizopigwa, mashambulizi ya hapa na pale yamekuwa yakishuhudiwa. Katika uwanja wa wa ndege wa mjini Donetsk mashambulizi ya hapa na pale yamekuwa yakishuhudiwa kutokana na umuhimu wa eneo hilo, limekuwa likishuhudia mashambulizi. Mjini Donetsk, kiongozi mkuu wa vikosi vya ulinzi wa uwanja wa ndege ameuawa jana Jumapili.

Kwa mujibu msemaji wa jeshi la Ukraine Andriy Lysenko, makundi yasio dhibitiwa nduo yamekuwa yakitekeleza mashambulizi. Ujumbe wa kijeshi wa Ukraine, Urusi na ule wa vikosi vya jumuiya ya ulinzi ya ukanda wa Ulaya mashariki wanajaribu kupitia hali ya mambo. Kiongozi huyo amesema miezi mitatu baada ya matumaini yaliotolewa katika makubaliano ya Minsk, hakuna kina hakikisha kwamba wananchi wa eneo la Donbass wanahitaji amani ya kudumu.