Kampeni za uchaguzi wa bunge kuanza wakati mashariki mwa Ukraine vita vikiarifiwa kuchacha
Imechapishwa: Imehaririwa:
Baada ya mzozo na Urusi wa takriban miezi saba, Ukraine imeanza kampeni za uchaguzi wa bunge jipya, uchaguzi ambao unafanyika chibi ya sera za rais anaegemea upande wa Ulaya, Petro Porochenko wakati huu kukiarifiwa kuendelea kwa mapigano hii leo mashariki kwa nchi hiyo.
Vyama vya siasa na wagombea ubunge wamepewa muda wa hadi saa sita usiku kuwasilisha majina kwenye tume ya uchaguzi, wakati huu kampeni zikianza kwa ajili ya uchaguzi wa Octoba 26. Katika nchi hiyo yenye kukabiliana na vita, uchaguzi huo hautofanyika katika maeneo ambao yapo chini ya udhibiti wa waasi.
Licha ya kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha vita yaliofikiwa Septemba 20 mjini Minsk kati ya serikali za kiev na Moscou, waasi pamoja na shirika la Usalama na ushirikiano barani Ulaya, mapigano yameendelea kushuhudiwa katika maeneo ya Uwanja wa ndege wa mjini Donetsk, moja miongoni mwa miji ilio chini ya udhibiti wa waasi.
Mjini Popasna katika mkoa wa Lougansk, uvurumishianaji wa roketi kati ya jeshi na waasi umesababisha vifo vya watu kadhaa na kuwajeruhi wengine baada ya kushammbuliwa kwa gari la wagonjwa, gavana wa eneo hilo Guennadi Moskal amethibitisha.
Siku ya jana imeshuhudia mapigano makali kuwa kuhshuidiwa tangu yalipofikiwa makubaliano ya kusitisha vita Septemba 5 ambapo wanajeshi tisa walipoteza maisha pamoja na raia wanne.
Tangu kufikiwa makubaliano ya kusitisha vita takriban watu 57 wameshapoteza maisha mashariki mwa Ukraine, ikifia idadi ya watu 3.200 waliopoteza maisha tangu kuanza kwa mapigano mwanzoni mwa mwezi April.
Baada ya waasi kufanya mashambulizi ya nguvu mwezi Agosti, rais Porochenko alifikia uamuzi wa kukubaliana kusitisha mtuto wa bunduki na waasi wanaotaka eneo hilo kujitenga na Ukraine na kuwa eneo la Urusi. Kutokana na hatuwa hiyo bunge la taifa hilo lilitowa makataa maalum kuhusu eneo linalo milikiwa na waasi, jambo ambalo lilitupiliwa mbali na waasi.
Waasi wanaopambana na serikali ya Urusi wamepinga kushiriki kwenye uchaguzi, na badala yake wameanda uchaguzi utaofanyika Novemba 2 mwaka huu.