UTURUKI-BUNGE

Bunge la Uturuki kupiga kura kuidhinisha mchango wake kwa vikosi vya muungano

wapiganaji wa Kikurdi 30/09/2014.
wapiganaji wa Kikurdi 30/09/2014. REUTERS/Murad Sezer

Kikao cha Bunge la Uturuki kinajadili hii leo faraghani kuhusu pendekezo liliwasilishwa la kuidhinisha uingiliaji kijeshi wa serikali ya nchi hiyo katika vita dhidi ya wapiganaji wa kiislam wa Islamic State nchini Iraq na Syria. Wapiganaji wa Kiislam wameyateka maeneo kadhaa karibu na mpaka wa Uturuki na Syria na kutishia kuuteka mji wa Kikurdi wa Ain-al Arab mpakani na Uturuki.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya kiislam ya Ankara inasema ipo tayari kutowa mchango wake katika vita dhidi ya kundi la IS. Hata hivyo haijawekwa bayana kuhusu ushirika wake katika muungano wa kimataifa kulipiga vita kundi hilo la kijihadi.

Hayo yanajiri wakati huu kundi la islamic State, likisonga mbele kwenye uwanja wa mapambano kuelekea kuuteka mji wa Kobane, licha ya mashambulizi ya vikosi vya muungano yanayoendelea.

Uturuki imeweka vifaru karibu na mpaka wake na Syria kuzuia mashambulizi ya IS, le 29/09/14.
Uturuki imeweka vifaru karibu na mpaka wake na Syria kuzuia mashambulizi ya IS, le 29/09/14. REUTERS/Murad Sezer

Wapiganaji wa Kikurdi wanaopambana katika mji huo muhimu kaskazini mwa Syria mpakani na Uturuki wapo tayari kwa makabiliano ya ndani kwa ndani iwapo IS watafaulu kuuteka mji huo wa Ain al-Arab kwa Kikurdi Kobane.

Shirika la haki za binadamu nchini Syria la OSDH linahofia kutokea kwa vitendo vya unyanyasaji kwa wananchi waliosalia katika mji huo iwapo utaanguka mikononi mwa kundi la Islamic State.

Islamic State wanasonga mbele kupitia eneo la kusini na mashariki ambako wapiganaji wa Kikurdi wameondoka katika maeneo mengi na kurejea kuulinda mji huo.

Kwa sasa wapiganaji hao wa kijihadi wapo kwenye umbali wa kilometa 2 pekee na mji huo. Shirika la haki za binadamu linasema kuna hofu ya kundi hilo kuuteka mji huo kwa muda wowote, lakini pia hofu ni uwezo wa wapiganaji wa Kikurdi kuulinda mji huo.

Wapiganaji wa IS ambao sasa wapo mlangoni mwa mji wa Kobane wanapambana vikali na wapiganaji wa Kikurdi ambao hawana uwezo mkubwa wa Kijeshi, wakati wapigananji wa IS wakiwa na silaha nzito nzito.