UTURUKI-PKK-Mapigano-Usalama

Jeshi la Uturuki laendesha mashambulizi dhidi ya waasi wa PKK

Mpikanaji wa kundi la PKK katika milima nchini Uturuki, karibu na mpaka wa Iraq (2013).
Mpikanaji wa kundi la PKK katika milima nchini Uturuki, karibu na mpaka wa Iraq (2013). AFP PHOTO/FIRAT NEWS AGENCY/STR

Ndege za jeshi la Uturuki zimeshambulia Jumatatu jioni wiki hii ngome za waasi wa kikurdi wa (PKK) kusini mashariki mwa Uturuki, jeshi la Uturuki limethibitisha.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo ni ya kwanza baada ya serikali na waasi hao kutia saini kwenye mkataba wa usitishwaji wa mapigano mwezi Machi mwaka 2013.

Mashambulizi hayahusiane na hali inayojiri wakati huu katika mji wa Kobane hususan kwenye mpaka wa uturuki na Syria, ambapo raia wengi wakikurdi wamelazimika kuyahama makaazi yao kufutia jaribio la wapiganaji wa Dola la Kiislam la kuudhibiti mji wa Kobane.

Ni kwa siku ya tatu sasa tangu Jumamosi, ngome ya wapiganaji wa kikurdi kwenye mpaka na Iraq imekua ikilengwa na mashambulizi ya roketi, bila hata hivo kusababisha maafa. Jeshi la Uturuki limeanzisha mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za wapiganaji wa kikurdi (PKK), na kusababisha hasara kubwa, kulingana na tangazo liliyotolewa na jeshi mapema leo asubuhi.

Operesheni hiyo dhidi ya waasi ni ya kwanza tangu miaka kadhaa iliyopita. Wiki iliyopita, kiongozi wa waasi Abdullah Ocalan aliitahadharisha serikali ya Uturuki kwamba iwapo hakutakua na utashi wa serikali wa kuendelea na mazungumzo hadi Oktoba 15 yaani Jumatano wiki hii, waasi wa PKK watajiondoa kwenye meza ya mazungumzo, na wataamua kuanzisha upya mapigano dhidi ya utawala wa Ankara.