UKRAINE-DONETSK-LUGANSK-Uchaguzi_siasa

Mashariki mwa Ukraine: Zakhartchenko achaguliwa kuwa rais Donetsk

Alexandre Zakhartchenko alionekana kuwa atashinda uchaguzi huo katika eneo Donetska liliyojitenga na Ukraine.
Alexandre Zakhartchenko alionekana kuwa atashinda uchaguzi huo katika eneo Donetska liliyojitenga na Ukraine. REUTERS/Maxim Shemetov

Raia wa maeneo yaliyojitenga mashariki mwa Ukraine wamepiga kura Jumapili Novemba 2 wakiwchagua marais wa maeneo hayo. Kulingana na matokeo ya uchaguzi “Waziri mkuu” katika eneo liliyojitenga la Donetsk, Alexandre Zakhartchenko, amechaguliwa kuwa rais kwa asilimia 81.37 ya kura.

Matangazo ya kibiashara

Raia wa eneo liliyojitenga mashariki mwa Ukraine wamepiga kura Jumapili Novemba 2 wakimchagua rais wa eneo hilo. Kulingana na matokeo ya uchaguzi “Waziri mkuu” katika eneo hilo liliyojitenga, Alexandre Zakhartchenko, amechaguliwa kuwa rais kwa asilimia 81.37 ya kura.

Alexandre Zakhartchenko, mwenye umri wa miaka 38, alikua akiongoza kundi moja la waasi, kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri mkuu wa eneo liliyojitenga la Donetsk.

Igor Plotnitski, mwanajeshi wa zamani, ndiye amechaguliwa kuwa rais katika eneo la Lougansk ililiyo jitenga pia na Ukraine.

Igor Plotnitski alituhumiwa na vyombo vya sheria vya Ukraine kumtuma Urusi rubani wa kijeshi wa Ukraine, Nadia Savtchenko, aliye kamatwa na waasi wakati wa mapigano mashariki mwa Ukraine. Rubani huyo mpaka sasa bado anazuiliwa nchini Urusi.

Vyama vya watu hao wawili vinaonekana kuwa vitashinda uchaguzi wa wabunge utakao fanyika hivi karibuni.

Mfululizo huu wa uchaguzi, ambao unadaiwa na serikali ya Kiev kuwa ni "uchaguzi wa ujanja" unalaniwa na nchi za Ulaya na Marekani. lakini Urusi imesema imeheshimu matokeo ya uchaguzi.

Mashirika ya kimataifa hayakutuma waangalizi katika uchaguzi huo. Lakini serikali za mitaa, ziliwaleta waangalizi wao kutoka vyama vya mrengo wa kulia kutoka Ulaya, waangalizi ambao Kiev imesema haiwatambui.