UKRAINE-DONETSK-LUGANSK-Uchaguzi_siasa

Uchaguzi Donetsk: pigo kubwa kwa umoja wa Ukraine

Alexandre Zakhatchenko (katikati) amechaguliwa kuwa rais wa eneo liliyojitenga la Donetsk kwa asilimia zaidi ya 80 ya kura.
Alexandre Zakhatchenko (katikati) amechaguliwa kuwa rais wa eneo liliyojitenga la Donetsk kwa asilimia zaidi ya 80 ya kura. REUTERS/Maxim Zmeyev

Rais wa Ukraine Petro Poroshenko leo Jumanne Novemba 4 atakutana na wakuu wa usalama nchini humo baada ya uchaguzi unaolezwa kutokuwa halali na serikali ya Kiev mashariki mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na raia wa Ukraine kupitia televisheni ya taifa, rais Poroshenko ameeelezea masikitiko yake kuhusu kufanyika kwa uchaguzi wa wawakilishi katika majimbo ya Donestsk na Lugansk, uchaguzi aliosema unarudisha nyuma juhudi za upatikanaji wa amani ya kudumu kati yake na Urusi.

Katika uchaguzi huo, viongozi wawili wanaoungwa mkono na serikali ya Urusi waliibuka washindi, uchaguzi uliosifiwa na Urusi na kukashifiwa na Ukraine pamoja na mataifa ya magharibi yakiongozwa na Marekani.

Rais Poroshenko, amesititiza kuwa Ukraine haiwezi kutambua matokeo ya viongozi wa majimbo hayo mashariki mwa nchi hiyo, kwa sababu umekiuka makubaliano ya kimataifa ya amani kati ya Ukraine, Urusi pamoja na waasi na katiba ya nchi hiyo.

Mapigano kati ya wanajeshi wa Ukraine na waasi wanaoiunga mkono serikali ya Urusi mashariki mwa nchi hiyo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu nne tangu yalipoanza kushuhudiwa mwaka huu.