UKRAINE-URUSI-N ATO-Usalama

Ukraine: Nato yathibitisha kuingia kwa wanajeshi wa Urusi, Moscow yakanusa

Magari ya kijeshi karibu na randabautiya mji wa Donetsk, mashariki mwa Ukraine.
Magari ya kijeshi karibu na randabautiya mji wa Donetsk, mashariki mwa Ukraine. REUTERS/Maxim Zmeyev

Ukraine inajiandaa kwa vita ili kujibu uchokozi wa Urusi wa kuivamia kijeshi baada ya wanajeshi wake kuonekana mashariki mwa nchi hiyo. 

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa kujihami wa nchi za magharibi Nato umethibitisha kuwa magari mengi ya kijeshi yalionekana siku za hivi karibuni kwenye msafara uliyokua ukitokea Urusi ukielekea mashariki mwa Ukraine. Moscow imebaini kwamba tuhuma hizo “hazina msingi”.

Kwa mujibu wa mkuu wa vikosi vya Nato, msururu wa magari ya kijeshi pamoja na wanajeshi wa Urusi wali walionekana mnamo siku mbili zilizopita wakivuka mpaka na kuingia mashariki mwa Ukraine, eneo linalodhibitiwa na waasi.

Viongozi wa Ukraine wamesema wamekua wakishuhudia hali hiyo, na kwa sasa wamajiandaa kwa vita dhidi ya kile walichokiita uvamizi wa majeshi ya kigeni.

Hata hivo msemaji wa wizara ya ulinzi ya Urusi, amekanusha tuhuma hizo, akithibitisha kwamba ni tuhuma zisiyo na msingi wowote, na kuituhumu Nato kuendelea kulichafua jeshi la Ukraine.

Msemaji huyo wa wizara ya ulinzi ya Urusi amebaini kwamba hivi karibuni kumekua kukionekana wanajeshi wengi wa kigeni kwenye mipaka ya Urusi, bila hata hivo kutoa taarifa zaidi. Ameendelea kusema kwamba ikihitajika wanajeshi watatumwa kwenye mipaka ya Urusi na jimbo la Crimea iwapo kutaoneka hali ya tahadhari.