Ukraine: Urusi yakanusha tuhuma dhidi yake
Imechapishwa:
Serikali ya Urusi imekanusha na kutupilia mbali madai ya nchi za magharibi kuwa inaendelea kupeleka vifaa zaidi vya kijeshi mashariki mwa Ukraine.
Mataifa ya magharibi yamebaini hivi karibuni kwamba mwenendo huo wa Urusi unaweza kuchochea mgogoro uliopo baina ya Ukraine na waasi waliojitenga.
Kauli hii ya urusi imetolewa baada kamanda wa majeshi ya kujihami ya nchi za magharibi NATO kutoa kauli ya kuishutumu Urusi kwa kupeleka vikosi na vifaa vya kijeshi nchi Ukraine.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Urusi, Alexander Lukashevich ameviambia vyombo vya habari kuwa hakuna wanajeshi wao wanaopigana nchini Ukraine kama ambavyo imekuwa ikidaiwa na nchi za magharibi.
Hivi karibuni viongozi wa Ukraine walisema wamekua wakishuhudia hali hiyo, na kwa sasa wamejiandaa kwa vita dhidi ya kile walichokiita uvamizi wa majeshi ya Urusi.