UFARANSA-MATEKA-UHURU-Jamii

Mateka wa mwisho wa Ufaransa awasili Paris

(kusoto kwenda kulia), Serge Lazarevic, waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian na rais wa Ufaransa François Hollande katika uwanja wa ndege wa Villacoublay, Desemba 10 mwaka 2014.
(kusoto kwenda kulia), Serge Lazarevic, waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian na rais wa Ufaransa François Hollande katika uwanja wa ndege wa Villacoublay, Desemba 10 mwaka 2014. REUTERS/Philippe Wojazer

Mateka wa mwisho wa Ufaransa, Serge Lazarevic, mwenye umri wa miaka 51 amewasili Jumatano Desemba asubuhi nchini Ufaransa, akitokea Niger. 

Matangazo ya kibiashara

Serge Lazarevic, alikua akishikiliwa mateka kwa kipindi cha miaka mitatu na kundi la Aqmi lenye mafungamano na kundi la Al Qaeda, kabla ya kuachiliwa huru Jumanne Desemba 9 mwaka 2014.

Alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Villacoublay, Serge Lazarevic amepokelewa na rais wa Ufaransa François Hollande na ndugu pamoja na jamaa zake.

Serge Lazarevic, alikua mateka wa mwisho wa Ufaransa duniani.

Wakati huohuo rais Hollande amewataka raia wa Ufaransa kutotembelea maeneo hatari, kwani raia wa Ufaransa wamekua wakilengwa na makundi ya kigaidi duniani.

" Kwa ndugu zetu wananchi ambao wanaweza wakajisahau na kujikuta katika maeneo hatari, fanyeni kinachowezekana ili msitembelei katika maeneo ambayo mnaweza kutekwa nyara. Tuko katika dunia hatari. Kuna maeneo ambapo hairuhusiwi kutembelea au kusafari. Huu ni utaratibu. Tunajua kwa sasa hali ya hatari inayojiri", amesema François Hollande mbele ya vyombo vya habari.

Kwa upande wake Serge Lazarevic amebaini kwamba kuwa mateka ni jambo lisilokuwa la kawaida.

“ Ni vizuri kuona narudi kuiona familia yangu na ndugu na jamaa. Sikudhani kuwa ntarudi kuwaona wapendwa wangu. Nilisahau kuwa uhuru upo, na kuwa huru ni bahati”, amesema Serge Lazarevic

Serge Lazarevic amemalizia akisema: " Nakushuruni kuwa mko hapa, nasema mara nyingine tena asanteni, nawashuru raia wa Ufaransa, naishukuru serikali, ambayo kila juhudi ili niweze kuachiliwa huru, nakushukuruni nyote”.

Serge Lazarevic, aliye kua mateka wa mwisho wa Ufaransa akitokea ndani ya ndege iliyomsafirisha nchini Ufaransa, Desemba 10  katika uwanja wa ndege wa Villacoublay.
Serge Lazarevic, aliye kua mateka wa mwisho wa Ufaransa akitokea ndani ya ndege iliyomsafirisha nchini Ufaransa, Desemba 10 katika uwanja wa ndege wa Villacoublay. AFP PHOTO / MARTIN BUREAU