Israeli yailaumu Mahakama ya Ulaya
Imechapishwa: Imehaririwa:
Israel imelani vikali uamuzi wa Mahakama ya Ulaya ya kuondoa Hamas katika kwenye orodha ya mashirika ya kigaidi kwa sababu ya hitilafu za kiutaratibu.
Orodha hii nyeusi iliwekwa baada ya mashambulizi ya Septamba 11 mwaka 2001 nchini Marekani. Kuna makundi mengi yanayojihusisha na ugaidi, ambayo yaliwekwa kwenye orodha hiyo, kama Hamas na tawi lake la kijeshi, ambavyo vilihusika na mashambulizi yaliyowalenga raia wa kawaida wa Israel.
PM Netanyahu: We're not satisfied w/ the EU's explanation that the removal of Hamas from its list of terrorist orgs is a 'technical matter'>
— PM of Israel (@IsraeliPM) December 17, 2014
Akihojiwa na RFI, mwanadiplomasia wa Ulaya mjini Brussels amesema kuwa hakuna mtu aliye unga mkono uamuzi wa Mahakama hiyo ambao umeibua utata.
Tume ya Umoja wa Ulaya imebaini kwamba itaendelea kuichukulia Hamas kama kundi la kigaidi na kubaini kwamba uamuzi wa Mahakama ya Ulaya uliyochukuliwa Jumatano wiki hii hauleti mabadiliko yoyote kwa msimamo wa kisiasa wa nchi 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya.
Umoja wa Ulaya umesema utakata rufaa ndani ya miezi mitatu, na kwa wakati huo, mali ya kundi hilo la Hamas zitaendelea kuzuiliwa.
Mashambulizi ya miaka 1990 na 2000 ndio yalipelekea Hamas kuwekwa kwenye orodha ya Umoja wa Ulaya ya makundi ya kigaidi . Nchi za magharibi haziungi mkono Hamas, licha ya ushindi wake katika uchaguzi wa wabunge uliyofanyika mwaka 2006.
Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Marekani na Urusi viliiwekea Hamas masharti matatu ili iweze kuwa mshirika wao wa karibu. masharti hayo ni pamoja na kuachana na vurugu, kuitambua Israeli na kutambua mikataba iliyoafikiwa kati ya Israel na Palestina. Masharti ambayo Hamas ilifutilia mbali.