UKRAINE-DONETSK-UFARANSA-URUSI-LUGANSK-Uchaguzi-siasa

Mazungumzo ya amani yatazamiwa kuanza Ukraine

Rais wa Ufaransa, François Hollande akieleza kuhusu mkutano wa amani unaotarajiwa kuanza wiki ijayo Ukraine.
Rais wa Ufaransa, François Hollande akieleza kuhusu mkutano wa amani unaotarajiwa kuanza wiki ijayo Ukraine. AFP PHOTO / THIERRY CHARLIER

Rais wa Ufaransa François Hollande amesema kuwa mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Ukraine na waasi wanaounga mkono hatua ya kujitenga huko mashariki mwa nchi hiyo yanatarajiwa kuanza jumapili hii au jumatatu wiki ijayo.

Matangazo ya kibiashara

François Hollande amesema kuwa mazungumzo hayo yatafanyika katika mji wa Minsk na utazikutanisha pande zinazohasimiana pamoja wa washirika wengine wa siasa za Ukraine.

Katika hatua nyingine Rais huyo wa ufaransa amesema kuwa mazungumzo ya simu ya yeye na rais Vladimir Putin, rais wa Ukraine Petro Poroshenko na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, yataendelea tena kuanzia jumanne kwa lengo la kusaka amani nchini Ukraine.

Hayo yanakuja wakati huu Urusi ikiendelea kunyoshewa kidole cha lawama na mataifa ya magharibi kuchochea machafuko na mgawanyiko nchini Ukraine hatua ambayo imekuwa ikipingwa vikali na Urusi ambayo inakabiliwa na vikwazo kuibana ibadili msimamo.