UKRAINE-JERMANI-URUSI-MAZUNGUMZO

Mazungumzo ya amani Ukraine yasuasua

Balozi wa Urusi nchini Ukraine, Mikhail Zurabov, akitoka ndani ya gari lake na kwenda kushiriki mazungumzo katika mji wa Minsk, tarehe 24 Desemba 2014.
Balozi wa Urusi nchini Ukraine, Mikhail Zurabov, akitoka ndani ya gari lake na kwenda kushiriki mazungumzo katika mji wa Minsk, tarehe 24 Desemba 2014. REUTERS/Stringer

Hakuna maendeleo yoyote kuhusu mazungumzo ya amani nchini Ukraine yaliyofanyika Jumatano Desemba 24 katika mji wa Minsk, kati ya serikali ya Kiev na waasi wa mashariki wanaotaka kujitenga.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo hatua ya kwanza imefikiwa kuhusu kubadilishana wafungwa. Tangazo hilo lilitolewa Alhamisi jioni Desemba 25 mwaka 2014 na waasi wa mashariki mwa Ukriane wanaotaka kujitenga.

Mkutano ambao umekua umepangwa kufanyika leo Ijumaa Desemba 26, haujaelezwa iwapo utaahirishwa au la.

Wajumbe wa waasi wanaotaka kujitenga na Ukraine walibaini Jumatano Desemba 24 baada ya mkutano huo kwamba mazungumzo kati yao na serikali yalikumbwa na mgawanyiko, na hivyo kupelekea mazungumzo hayo kusitishwa.

Wajumbe hao wa waasi wamebaini kwamba mkutano wa pili uliyokua umepangwa kufanyika Ijumaa Desemba 26 mwaka 2014, hatimaye umefutwa.

" Kama duru ya pili ya mazungumzo itakua bado haijathibitishwa kufanyika kwa muda uliyopangwa, angalau makubaliano yalifikiwa Jumatano Desemba 24 mwaka 2014 kwa kubadilishana wafungwa", waasi wanaotaka kujitenga wamethibitisha.

Raia 225 wa Ukraine wanaozuiliwa na waasi wa mashariki mwa Ukraine wanatazamiwa kuachiliwa huru dhidi ya waasi 150 wanaozuiliwa jela na viongozi wa Ukraine.

Viongozi wawili wa jamhuri za waasi wanaotaka kujitenga za Donetsk na Lugansk wamelifahamisha shirika la habari la Urusi Ria Novosti kwamba zoezi hilo la kubadilishana wafungwa huenda likafanyika mwishoni mwa wiki hii. Alhamisi Desemba 16 jioni, Kiev ilikuwa haijathibitisha tangazo hilo la waasi.