Pata taarifa kuu

Vyombo vya habari nchini Ufaransa vyashirikiana pamoja katika kuomboleza

Jarida la vibonzo la Charlie Hebdo lilishambuliwa na magaidi na kuwaua watu 12, Jumatano Januari 7 mwaka 2015.
Imehaririwa: 09/01/2015 - 10:13

Mimi ni Charlie,Jumatano wiki hii mjini Paris, shambulio la kigaidi liliendeshwa dhidi ya Jarida la Charlie Hebdo. Watu kumi na wawili waliuawa. Waandishi wa habari, askari polisi, marafiki. Kwa niaba ya makundi yote ya vyombo vya habari nchini Ufaransa, tunatoa salamu za rambirambi kwa familia zao, kwa wale ambao walitutoka na timu nzima ya jarida Charlie Hebdo. Kupitia kwao ni uhuru wa vyombo vya habari na, muhimu zaidi, uhuru ambao umepata pigo kubwa.Vyombo vya habari vimepigwa na simanzi kwa kile kilichotokea kwa ndugu zao. Vyombo vya habari vinatualika tuwe na ucheshi na kujizuia na utengano na kuwa na mshikamano. Wale ambao wametutoka Jumatano wiki hii wametuachia ucheshi katika nafsi zetu kwa kutufanya tuwe na uhuru zaidi. Kila mara, uhuru wa mawazo na uhuru wa kujieleza ndio vigezo vya kazi yetu ya kila siku.Katika siku hii ya maombolezo, tunatumia fursa hii kuhakikisha kuwa hatutakubali vitisho wala kuhofiwa maisha yetu kwa vyovyote vile. Hatutasalia kimya, nasi tutapiga vita dhidi ya kila aina ya ubaguzi.Vyombo vyote vya habari vya Ufaransa vimejipanga kwa hali na mali kuhakikisha jarida la vibonzo Charlie Hebdo linaendelea kuishi.Sote kwa pamoja tumeshirikiana ili kutetea uhuru wa vyombo vya Habari. Na tutaendelea kuutetea kwa niaba yao.Waliosahini Tangazo hilo:Christopher Baldelli (RTL), Christophe Barbier (L'Express), Jean-Paul Baudecroux (NRJ), Pierre Bellanger (SKYROCK),  Jérôme Bellay (Le Journal du Dimanche), Nicolas Beytout (L’Opinion), Véronique Cayla (ARTE), Matthieu Croissandeau (L’Obs), Nicolas de Tavernost (M6), Bruno Delport (Nova), Louis Dreyfus (Le Monde), Marc Feuillée (Le Figaro), Mathieu Gallet (Radio France), Etienne Gernelle (Le Point), Emmanuel Hoog (AFP), Jean Hornain (Le Parisien),Patrick Le Hyaric (L'Humanité), Gérard Leclerc (LCP-AN), Gilles Leclerc (Public Sénat), Bertrand Meheut (CANAL+), Francis Morel (Les Echos), Denis Olivennes (Lagardère Active / Europe 1), Nonce Paolini (TF1), Fabienne Pascaud (Télérama), Rémy Pflimlin (France Télévisions), Matthieu Pigasse (Les Inrockuptibles), Dominique Quinio (La Croix),  Olivier Royant (Paris Match), Marie-Christine Saragosse (France Médias Monde), Jean-Christophe Tortora (La Tribune), Jean-Eric Valli (Les Indés Radio),  Maurice Szafran (Le Magazine  Littéraire), Alain Weill (NextRadioTV)Thomas Legrand-HedelNaibu mkurugenzi wa MawasilianoDirecteur adjoint de la CommunicationDeputy director of Communications

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.