UKRAINE-DONETSK-Mapigano-Usalama

Mapigano yaripotiwa Donbass

Watu waliojitolea kuungana na jeshi dhidi ya waasi nchini Ukraine waapishwa katika kambi iliyo chini ya  wizara ya Mambo ya Ndani, Januari 17, mwaka 2015.
Watu waliojitolea kuungana na jeshi dhidi ya waasi nchini Ukraine waapishwa katika kambi iliyo chini ya wizara ya Mambo ya Ndani, Januari 17, mwaka 2015. REUTERS/Gleb Garanich

Baada ya vikosi vya Ukraine kudhibiti sehemu ya zamani ya uwanja wa ndege wa Donetsk, pande zote mbili husika katika mgogoro unaoendelea Ukraine, ikiwa ni jeshi na waasi, zinaonekana kuwa na nia ya kuendelea na vita, wakati mazungumzo ya amani yakishindikana.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI katika mji wa Kiev, Sébastien Gobert, picha za mabaki ya magari ya kijeshi katika uwanja wa ndege wa Donetsk zinatisha. Hata hivyo hali katika uwanja wa ndege wa zamani wa Donetsk imekua ni tete, ingawa inaonekana kwamba mashambulizi ya vikosi vya Ukraine dhidi ya waasi yalifikia malengo yake.

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi, eneo la uwanja wa ndege lililopewa raia wa Ukraine katika mazungumzo ya amani " limewekwa kwenye himaya ya jeshi la serikali". Kila upande umerudi katika ngome zake uliyokua ukishikilia wiki moja iliyopita.

Mashambulizi ya anga yanaendelea karibu na mji wa Donetsk na mahali pengine katika mji wa Donbass, na huenda hali ikabadilika. Mshauri wa rais Poroshenko amesema wako tayari " kuwang'oa meno" waasi. Viongozi wa wa jimbo la Donetsk wamesema kwa upande wao wako tayari kuendelea na mapigano ikiwa itahitajika.

Wakati huo huo, pande zote zinasema ziko tayari kwa mazungumzo mapya. Hata hivyo jaribio la tatu la kusitisha mapigano katika mji wa Donbass limegonga mwamba.